Msikie Zlatan Baada ya Soka…

Miongoni mwa wachezaji ambao wameweza kujijengea heshima kubwa sana katika soka ni Ibrahimovic kutokana na kuyaishi maisha yake halisi katika ubora, uwezo na hata kutumia mbinu zake zote kuzipa ushindi timu alizokuwa nazo katika maisha yake ya kisoka kwa kipindi chote.

Kwa sasa anakipiga La Galaxy akiwa katika harakati za kukusanya mafao yake ndani ya ligi hiyo lakini akiwa tayari na umri mkubwa ameweka bayana juu ya lini hasa ataaga maisha hayo ya soka na kuishi maisha mengine kama wengine.

Imekuwa kawaida kwa wakongwe wa soka kuzihama ligi zenye ushindani mkubwa na kuelekea katika ligi ambazo hazina ushindani mkubwa ikiwa na lengo la kutengeneza hela kwa kipindi hicho, japo wengine hufanya hivyo ikiwa ni sehemu ya mapenzi yao na soka kwa kuona ugumu kuzihama klabu zao kwa wakati huo jambo ambalo umri pekee huwa kikwazo kwao kuhama.

Kwake Ibrahimovic ambaye amechezea klabu kubwa kama PSG, United na Barcelona msimu huu unaweza ukawa wa mwisho kwake baada ya kufaidi kila lililo jema mbele yake na kuondoka na vikombe vingi sana kwenye maisha yake ya soka jambo ambalo anajivunia kulifikia ambapo wengi hutamani pia.

Alipoulizwa juu ya kitu gani angependelea kukifanya baada ya kuachana na soka, aliweka wazi kwamba anatamani sana kama angejiunga na wacheza filamu ili aweze kuuvaa uhusika fulani kwa sababu kwa sasa akistaafu haangalii tena kujiunga na ligi yoyote ile ya soka.

Anatamani awe muigizaji ili aruke hapa na pale katika majengo marefu ili kutokana na nafasi hiyo aweze kutimiza lengo lake hilo ambalo alikuwa akitamani kulifanyia kazi kwa muda mrefu sana. Uhusika huo unamfaa kabisa kwa sababu umri wake bado unamruhusu kuyafanya hayo jambo ambalo halileti wasiwasi kwake.

Katika sehemu yake ya mafanikio ni kuweza kufikisha idadi ya magoli 500 katika historia yake ya maisha ya soka na anapewa heshima yake kubwa kwa hatua hiyo ya pekee na ya kihistoria. Wengi sana wanatamani kupafikia hapo lakini ni wachache wanapata nafasi kupafikia; anaungana katika nafasi hiyo na wachezaji wengine kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambao wamefikia kiwango hicho.

Ibrahimovic hataki mbegu yake ipotee, anajitahidi izaliane zaidi na kuleta kila alichokiacha yeye mbele ya uso wa wengi ili kufanya historia na mazuri yake yasipotee. Anachojivunia kwa sasa ni kuwafanya watoto wake kuchagua upande wake wa soka ambao umeweza kumjengea mafanikio kwa kiasi kikubwa.

Yeye anaona kwamba kile alichokifanya yeye kinakuja kwa awamu nyingine kwa wanawe hao, Maximilian na Vincent.

2 Komentara

    Kadabla mwamba sana

    Jibu

    Jeshi

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.