Barcelona wameripotiwa kukamilisha dili la kumsainisha kinda wa timu ya taifa ya Uingereza Louie Barry.
Staa huyu mtoto aliyekuwa West Brom alikuwa akihusishwa na kwenda Ligue 1 kwa klabu ya Paris Saint Germain, pia klabu zingine kadhaa za Ligi Kuu ya Uingereza zilikuwa zikimfukuzia.
Barca wamefanikiwa kuinasa sahihi ya kinda huyu wa miaka 16 ambaye amesaini mkataba wa miaka 3 kuitumikia klabu hiyo.
Kinda huyu ametumia miaka yake 10 akiwa na West Brom, na alianza rasmi kucheza mechi ya vijana chini ya miaka 23 msimu uliopita.



Elika
Hongera kwake barry..kwenda kuichezea Barcelona sio mchezo mchezo.hongera kwake kipaji kimeonekana
Ester jackson
Hongera sana Barry kwa kusajiliwa timu yenye uwezo mzuri
Povel
Gud news
Fatina mfingi
Makal nzur