Fununu za Usajili Ulaya

Ikiwa dirisha la usajili likiwa limefungwa nchini Uingereza lakini kuna maeneo ambako bado wapo sokoni kujenga vikosi vyao. Klabu ya Juventus bado ipo sokoni kuangalia klabu yoyote itakayomuhitaji nyota na raia wa Argentina, Dyabala ili kuwasaidia kupunguza gharama ndani ya kikosi chao. Klabu hiyo ipo tayari kufanya hivyo kwa klabu yoyote isipokuwa kwa majirani zao, Inter Milan.

Baada ya dili la Rojo kujiunga na Everton kushindikana imeleta sintofahamu kwa nyota huyo ambaye alidhamiria kutimka klabuni hapo kutokana na kuonelea kwamba atakosa namba ya kucheza ndani ya kikosi hicho. Maamuzi ya klabu yalikuwa ni kwamba nyota huyo aweze kupelekwa kwa mkopo kwa sababu United hawakuwa tayari kufanya biashara ya kumuondoa kabisa kikosini kwao mchezaji huyo.

Wilfred Zaha ameshindwa kusajiliwa na klabu yoyote nyingine msimu huu kutokana na usajili wake kuwekewa kigingi na matajiri wa klabu yake ambao walitumia kila mbinu kuziba mianya ambayo ingemuweka nyota huyo kuondoka klabuni hapo. Awali alikuwa anawindwa na Everton lakini ikawa ni vigumu kwake kuondoka kutokana na mahitaji ya kikosi chake kwa sasa.

Hazard baada ya kutua Madrid alikuwa akitumia jezi yenye namba 50 ndani ya kikosi hicho ambapo yalikuwa ni maandalizi ya klabu hiyo kuangalia namba ambayo ingeweza kumfaa nyota huyo ambaye walimsajili kwa ada nzito kutoka Chelsea. Kwa sasa amekabidhiwa jezi namba 7 iliyokuwa ikivaliwa na Ronaldo na ni jezi yenye heshima kubwa sana kikosini hapo. Hivyo ana jukumu la kuitumia vyema sana ili kuleta heshima zaidi.

Klabu ya Arsenal bado wapo katika harakati za kuangalia kama wanaweza kupokea ofa ya kuwauza baadhi ya nyota wao ambao kwa sasa wanaona kama klabu imepata mbadala wao tayari. Wachezaji kama Mustafi na Elney kwa sasa hawana nafasi kubwa sana kikosini hapo hivyo haina ugumu kwao kuweza kuwatafutia soko kwa sasa ili waweze kupigana nje ya klabu yao hiyo.

Kocha wa klabu ya Manchester United, Ole anaamini kwamba nyota wa klabu yao hiyo, Alexis Sanchez atakuwa na msimu mzuri kikosini hapo baada ya kumuingiza katika takwimu za wachezaji atakaokuwa nao msimu huu. Mbali na hilo, klabu ya Roma inaangalia uwezekano wa kumnasa hata kwa mkopo endapo Manchester United watakubaliana na dili hilo ambalo wao wanaamini litakuwa na manufaa kwao. Lakini kutokana na aina ya wachezaji ambao klabu ipo nao msimu huu itakuwa vigumu kumuondoa nyota huyo.

Makala iliyopita

2 Komentara

    Hii habari safi.

    Jibu

    Gud update

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.