Nyota wa mchezo wa tenisi duniani kutokana na uwezo wake na upinzani wake mkubwa kwa hakika ameweza kufikia hatua ambayo haishawishi kumuona akiwa katika hali hiyo ambayo inaashiria kuanza kupotezwa kwenye ramani ya ushindani na kuibua washindani wapya kwenye mashindano mengi makubwa yajayo.
Aliweza kurejea uwanjani akitokea majeruhi ambayo ameyatumikia kwa kipindi kirefu tangu Januari na kurejea wake kulikuwa na nia ya kutaka kuangalia kama angeweza kurejea kuleta ushindani lakini mambo yamekuwa tofauti kabisa na kile ambacho kilitazamiwa kwamba kingetokea kwenye mechi zake anazoingia uwanjani.
Murray alijikuta mpira wake wa mwanzo kabisa ukizuiwa na mpinzani wake raia wa Ufaransa, Richard Gasquet ambaye alionekana mwiba mkubwa sana kwa nyota huyo wa mchezo wa miaka mingi na kufanya kupoteza mechi yake mbele ya umati uliokuwa na nia ya kushuhudia kurejea kwake uwanjani.
Mbali na uwezo wa Murray lakini wawili hawa wote walikutana wakiwa wametokea majeruhi na ilikuwa ni nafasi ya kila mmoja kuonesha makali yake katika kipindi hiki ambacho wanarudi ulingoni wakitoka kuuguza majeraha yao ambayo waliyapata katika harakati za kupigana angalau wanyanyuke na vikombe.
Mechi ilionekana kuwa ngumu tofauti na vile ambavyo ilichukuliwa mara baada ya Mfaransa huyo kupata nguvu ya kuongoza zaidi na kuonekana mwenye mbinu zilizozidiana na zile ya Murray ambaye ni mkongwe wa mchezo huo. Kwa hatua hiyo sasa hatuwezi kumshuhudia katika michezo hiyo nyota huyo hivyo kwani ameaga mashindano tayari.
Kilichosalia kwa sasa ni nyota huyo kwenda kujifua zaidi baada ya kufanya vibaya na nje ya kiwango chake kwa msimu huu. Nia yake ya kupambana zaidi na kujipa muda wa maandalizi inaweza kumsaidia kwa namna ya pekee kumjenga na kujifunza zaidi kupitia kipigo hicho na mwisho ataweza kurejea kwenye kilinge akiwa imara zaidi.


isha
Duuh hatari sana
Povel
Habar njema
Furahav
Yuko vizuri.