Kama ilivyo ada klabu inakuwa na majina ambayo kwa hakika inadhamiria kuyashusha kikosini ili kukipa nguvu kikosi ikiwa na lengo kubwa lenye manufaa ya aidha kuweza kufikia malengo ya muda mrefu ya kikosi ambayo ni kunyanyua ubingwa au kuweza kuivusha timu kwenye janga la kushuka daraja katika msimu husika. Ufuatao ni usajili ambao umeweza kufanikiwa kwa sasa katika klabu nyingi za Uingereza:
David Luiz amefanikiwa kulazimisha uhamisho wake na kutimkia katika klabu ya majirani zao, Arsenal akitokea katika maamuzi ambayo hayakufikiriwa kabisa ikiwa yalikuwa ya haraka sana na yaliyoweza kuwashtua wadau wengi wa soka. Amejiunga na Arsenal kwa uhamisho wa ada ya £8m na atakuwa akitumia jezi namba 23 kwa msimu huu.
Nyota aliyekipiga na Arsenal msimu uliopita, Alex Iwobi ameweza kutimka kikosini hapo na kujiunga na Everton kwa uhamisho wa ada ya £40m akiwa bado mwenye kiwango cha aina yake ndani ya kikosi hicho cha wazee Washika Mitutu wa jiji la London. Huenda ukawa ni usajili mzuri sana kwa Everton msimu huu na wameweza kumfungia kwa mkataba wa miaka mitano ya kuhudumu kikosini hapo.
Klabu ya Leicester imefanya usajili wa nyota aliyekuwa akikipiga na Sampdoria, Dennis Praet katika usajili uliohusisha kiasi cha £18m ikiwa ni katika harakati za kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu huu. Nyota huyo ameweza kusaini kandarasi ya miaka mitano itakayomuweka klabuni hapo kwa miaka mitano zaidi.
Wababe wa klabu kubwa kwa msimu uliopita, Wolves wamefanya usajili wa kinda kutoka Bayern Munich, Meritan Shabani katika mkataba utakaomfanya asalie klabuni hapo kwa miaka mitatu. Ni usajili wa maana sana kwa kikosi hicho na watakuwa na makali kama yale ya msimu uliopita.
Kinda wa klabu ya Chelsea, Chalobah ameweza kupelekwa kwa mkopo katika klabu ya Huddersfield ikiwa ni hatua nzuri ya kuwapa vijana nafasi ya kukuza vipaji vyao na kujifunza mengi nje ya maeneo yao. Hiyo huwa ni nafasi ya pekee kwa wachezaji wachanga kama hao kuonekana zaidi mbali na pale walipo kwa wakati husika.
Crystal Palace wamemsajili James McCarthy kutoka Everton ili aweze kuhudumu nao kwa msimu huu wote. Nyota huyo amejiunga na klabu hiyo kwa usajili uliogharimu kiasi cha £8.5m na amesajiliwa akiwa bado na kiwango kikubwa na cha pekee sana ndani ya klabu hiyo.
Povel
Habar njema
Furahav
Iko vizuri.