Safari Njema Migne!

Timu ya taifa inapokuwa na matokeo mabovu mara nyingi lawama zote za wachezaji hutupiwa kocha hata katika wakati ambao siyo sahihi kwa kocha kuweza kupewa lawama hizo. Jambo kama hilo kwa namna fulani limekuwa la kawaida sana katika soka la Afrika ambapo kocha huangaliwa moja kwa moja kwa kila matokeo yanayopatikana.

Jambo hili limekuwa likiwaondoa makocha wengi sana wa kigeni katika bara la Afrika ambapo ni vigumu sana kwa kocha kuendana na mifumo ya kisoka iliyopo bila kupewa muda mwingi wa kuijenga timu na kuangalia aina ya wachezaji ambao wanaweza kufaa kwa kocha huyo kuwa nao kikosini.

Jambo hili hata kwa nchi za ukanda wa Afrika limeweza kutokea mara kadhaa kwa nchi kama Tanzania lakini kwa sasa limeweza kutokea nchi ya Kenya ambapo nao wameamua kuachana na aliyekuwa kocha wao katika michuano mbalimbali waliyoishiriki kwa siku za hivi karibuni na hata nyuma ya hapo.

Aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Sebastian Migne amekubaliana na taifa hilo kwa kunawa mikono na kukubali kuvunjiwa mkataba wake na uongozi wa klabu hiyo ikiwa ni mara moja kutokana na kutokuridhishwa na kiwango cha timu yao ya taifa kilichooneshwa katika siku za hivi karibuni.

Shirikisho la Soka la Kenya limefikia maamuzi hayo mara baada ya kutolewa na Tanzania kwenye michuano ya CHAN na kuona kwamba hakuna haja ya kuendelea kumkumbatia mwalimu huyo kwa wakati uliopo na kuamua kukaa naye katika makuBaliano ya kuvunjiwa mkataba wake.

Harambee Stars walitolewa kwa mikwaju ya penati wakiwa katika uwanja wa nyumbani ambapo walikuwa wanatafuta tiketi ya kushiriki michuano hiyo ambayo hushirikisha wachezaji wengi wanaocheza ligi za ndani ya nchi yao lakini walishindwa kabisa kupata nafasi ya kupenya ili kupata nafasi ya ushiriki katika michuano hiyo.

Sakata hili la kutimua makocha kwa kipindi kifupi linaweza kuwa ni ugonjwa unaosababisha soka la mataifa mengi hususan Afrika kurudi nyuma kwa sababu kila kocha huwa na mfumo wake ambao siyo rahisi kwa kocha kuupandikiza endapo atakaa kwa kipindi kifupi sana hivyo anahitaji muda ili kukipa nguvu na kuweka mbinu zitakazoendana na mifumo yake pamoja na jiografia ya soka letu lilivyo. Hivyo, makocha wetu huhitaji muda zaidi kupandikiza na kuzijenga timu zao.

Makala iliyopita

3 Komentara

    Walipaswa kuwapa makocha muda kabla yakuwakosoa

    Jibu

    Mmh makocha wanawakati mgumu sana.

    Jibu

    Mmhhmmhh

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.