Baada ya kupata ushindi mnono katika mechi ya ufunguzi wa ligi kwa idadi ya kutosha ya magoli na kikosi chake cha msimu uliopita kuonekana bado kipo imara zaidi kwa mapambano ya msimu huu mpya wenye ushindani wa kila aina ambapo kila mmoja amejizatiti kuondoka na ushindi wa mapema ndani ya ligi hiyo sasa klabu ya Liverpool imeingiwa na ugonjwa wake wa awali kabisa ambapo mlinda mlango wao tegemezi ambaye ameibeba klabu hiyo kwa msimu mzima kiushindani, Allison amepata majeraha ya mapema kabisa ambayo kwa hakika ni jipu kubwa sana na tatizo kubwa sana ndani ya kikosi hicho kwa msimu huu.
Allison amethibishwa kuumia na kwamba atakuwa nje ya kikosi hicho kwa kipindi kirefu zaidi baada ya kupata majeraha ambayo yamethibitishwa na kocha wa kikosi hicho kwamba hawezi kuwa na nyota huyo kwa sasa baada ya janga hilo lililotokea kwake na inaweza kuwa changamoto pamoja na kwamba wana mlinda mlango mwingine.
Hii inaweza kuwa siyo dalili nzuri kwa kikosi hicho ambacho msimu huu kinatafuta kurudisha heshima katika soka baada ya kutwaa ubingwa wa klabu bingwa na sasa anatafuta heshima ya kuweza kunyanyua ubingwa wa ligi hiyo ili kufuta uteja wake na kurejesha heshima ambayo ameikosa kwa kipindi kirefu sana.
Allison ni nguzo kubwa sana katika mafanikio ya kikosi hicho kwa msimu uliopita na anastahili heshima kubwa sana. Ameumia katika wakati ambao tunaweza kusema Liverpool inamuhitaji ili kuweza kuisaidia kunyanyua makombe ambayo ndiyo heshima ya pekee kwa kila kikosi ambacho kinatafuta mafanikio.
Liverpool mara kadhaa wakiwa katika malengo endelevu hukutana na mitihani kama hii ambayo huweza kupoteza kabisa muelekeo wa kikosi na isitoshe masuala haya yanaanza kutokea asubuhi na mapema ambapo mipango inakuwa ikisukwa. Tuzidi kuona kama majeraha ya mlinda mlango huyo hayataleta tatizo ndani ya kikosi hicho.
Japo kiuhalisia mechi kama ile dhidi ya Norwich haikuwa na ulazima wa nyota wote wa kikosi cha kwanza kuonekana uwanjani kutokana na mechi ambayo anakwenda kukabiliana nayo siku ya Jumatano dhidi ya Chelsea katika mchuano wake mgumu sana wa kujaribu kutetea taji jingine kubwa.

