Nyota mkongwe na raia wa Ureno, Christino Ronaldo ameweka wazi tofauti kubwa kati yake na mpinzani wake wa siku nyingi ili kujaribu kumaliza utofauti na ubora uliopo kati ya wawili hao na kuona kwamba wanaohangaika kuwalinganisha wao wana kitu wanachokosea na wanapaswa kuweka baadhi ya vitu ili kuweka sawa mambo.
Kitu ambacho Ronaldo anakiona ni ufahari kwake kumfanya bora zaidi ya mwenzake ni kwamba yeye ni mshindani zaidi kutokana na kunyanyua makombe yenye heshima likiwemo lile la klabu bingwa barani Ulaya na kombe hilo amenyanyua akiwa na klabu tofauti na siyo klabu moja kama ilivyo kwa mpinzani wake.
Uhasimu wake uliongezeka baada ya nyota huyo kuhamia Hispania akitokea Uingereza katika klabu ya Manchester United jambo ambalo lilichochea zaidi uimara wa wawili hao. Mbali na hilo, bado kila mmoja ana ubora katika eneo fulani ambalo mwingine hana ubora nalo. Hivyo, kila mmoja anakaa na kimoja kinachomlinda.
Suala la tuzo za Ballon d’Or halitoshi kabisa kuwatofautisha wawili hao kutokana na wawili hao kuwa na idadi sawa kabisa ambapo kila mmoja yupo sawa na mwenzake. Lakini linapokuja suala la kuchezea ligi nyingi tofauti kwa mafanikio makubwa basi, Ronaldo anaonekana imara kwa kuweza kuendana na ligi nyingi kwa mataji na mafanikio makubwa.
Baadhi ya mafanikio ya Ronaldo ambayo yanampa alama zaidi ni kuchezea klabu za Uingereza, Hispania na Italia kwa mafanikio na akafanikiwa kutwaa makombe yote yanayoitambulisha ama klabu au taifa fulani yakiwemo ya klabu bingwa, kombe la dunia la FIFA ngazi ya klabu, kombe la Ulaya akiwa na Ureno; hayo ni sehemu ya mafanikio makubwa sana kwake.
Lakini mpinzani wake amejiwekea heshima katika ligi lakini ameshindwa kuweka mambo sawa upande wa mataji ya nje ikiwemo katika ngazi ya taifa na hata ule ushindani wa nje ni suala ambalo amelikosa kabisa kwa sababu ameweza kukulia Hispania ndani ya Barcelona na anaonekana anaweza kustaafu akiwa ndani ya klabu hiyo.
Kiuhalisia siyo rahisi kupata jibu la moja kwa moja la ni nani anapaswa kuwa bora zaidi ya mwenzake lakini kikubwa ni kwamba wawili hao kila mmoja ana eneo ambalo siyo rahisi kuendana na mwenzake hivyo hakuna haja ya kuwaacha waendelee kupambanishwa kwa sasa.


Fatina mfingi
Ni kweli maan watu awawezi kuwa sawa kila mtu na ufundi wake uwanjan