Mapema wiki hii Liverpool waliweza kuandika historia kwa kunyanyua kombe la Super Cup lililowakutanisha mabingwa wa kombe la klabu bingwa msimu uliopita, Liverpool na mabingwa wa Europa, Chelsea ambapo ilishuhudiwa Majogoo wakifanikiwa kuweka kombe jingine kubwa katika makabati yao ya uhifadhi.
Ni kipindi kirefu tangu Majogoo walipofanikiwa kuwika sana katika soka na kunyanyua makombe jambo ambalo wameweza kufanikiwa kuvunja miiko hiyo kwa msimu huu pekee na kufanikiwa kunyanyua mataji hayo mawili mbele ya wapinzani wao wenye uwezo mkubwa na wa kipekee kabisa uwanjani.
Liverpool ndiyo walionekana kuutawala sana mchezo mbali na Chelsea kutengeneza mashambulizi mengi upande wa mpinzani lakini uimara wa safu ya ulinzi uliweza kuleta makubwa na jipya lilionekana kwamba muunganiko wao wa msimu uliopita ulikuwa na nafasi kubwa kwa mafanikio yao.
Chelsea ya Lampard haijawa na mwanzo mzuri katika mashindano yaliyo mbele yao baada ya kuwa ni klabu inayopoteza mara kwa mara ikiwa tayari imepokea vipigo viwili mbele ya klabu zinazotoka katika ukanda wao wa taifa la Uingereza. Jambo hilo linahatarisha endapo nyota hao wakiwa na kocha wao watafanikiwa kujizatiti kuifikia nafasi hata ya nne.
Mbali na kupoteza kombe hilo, Chelsea wameonesha ukomavu kwa kuwatumia wachezaji wengi wa ndani katika soka jambo ambalo kwa hakika linajenga kizazi halisi cha klabu hiyo ambacho kitaifikisha panapotakiwa kwa miaka ya baadaye kutokana na umri wao kulinganisha na umri walionao kwa sasa.
Endapo mwenendo wa kikosi utaendelea hivyo hatuoni kama Lampard ana maisha marefu ya kuvumiliwa na tajiri wake mbali ya kwamba yeye ni mtoto wa nyumbani. Siku zote mafanikio kwanza ndani ya timu ndicho kinachotakiwa kwa kikosi na klabu yenye jina kubwa na mapato kama Chelsea.
Ni msimu ambao utakuwa mgumu sana kwa Chelsea kutokana na kumiliki wachezaji tegemezi ambao bado hawajajua njaa ya goli inakuwaje na hatimaye kuharibu nafasi nyingi sana za magoli ya wazi ambayo yangewapeleka mbali na yangewafanya kushindana zaidi.
Povel
Gud news