Baada ya Virgil van Dijk kunyakua tuzo ya UEFA kama mchezaji wa mwaka kwa soka la wanaume, staa huyu tena ameingia kwenye hatua orodha ya 4 bora wanaowania tuzo nyingine Fifa.
Virgil van Dijk, alikuwepo pamoja na nyota wa zamani wa Real Madrid Christiano Ronaldo na Lionel Messi kwenye lala salama ya kinyang’anyiro cha tuzo za UEFA. Mastaa hawa wote wameingia pia kwenye fainali ya kinyang’anyiro cha tuzo za FIFA, -Best Fifa Footbal Award. Nyota wa Lyon Lucy Bronze naye yupo kwenye tuzo hii kama mchezaji bora wa kike.
Bosi wa Manchester City, Pep Guardiola, Jurgen Klop wa Liverpool na Mauricio Pochettino wa Tottenham Hotspurs wanachuana kutwaa tuzo ya kocha wa mwaka.

Alisson Becker wa Liverpool, Marc ter Stegen wa Barcelona na Ederson Morae wa Man City wanachuana kutwaa tuzo ya golikipa bora wa mwaka -FIFA.

Washindi wanatarajiwa kutangazwa Septemba 23. Inaweza kuwa shavu kwa Virgil van Dijk tena? huenda ikawa nafasi nyingine kwa staa huyu, lakini bado ana ushindani mkubwa kutoka kwa wakali Ronaldo na Messi, lolote linaweza kutokea.


Furahav
Namkubali sana,beki kisiki.
Gabriel
Wote wakal sana
Povel
Haki itendekeh