Klabu za Manchester United na Inter Milan zimefungua faili kwa mara nyingine juu ya usajili wa nyota wa klabu ya United na raia wa Chile ambapo Inter nia yao ni kutaka kumchukua nyota huyo kwa mkopo kwanza kutokana na gharama kubwa ambazo United wanazo juu ya nyota huyo. Nyota huyo anagharimu kiasi kikubwa akimalipo ikiwemo katika usajili na hata malipo ya mshahara ndani ya klabu hiyo tangu asajiliwe kutoka Arsenal.
Luis Fillipe ambaye amekipiga na klabu kama Chelsea na Atletico Madrid amezikataa ofa kubwa kutoka Manchester City, Lyon na Dortmund na kuamua kurudi zake nyumbani kwao Brazil ambako atakuwa na klabu ya Flamengo ikiwa ni hatua ambayo hufanywa na nyota wengi wa taifa hilo wanapofikia umri wa kustaafu kuamua kukimbilia katika ardhi yao ili kucheza huko ikiwa kama sehemu ya shukrani kwa maisha yao.
Kama ilivyokuwa ikisemekana hapo awali kwamba raia wa Kenya na mchezaji wa zamani wa klabu ya Tottenham amepewa mkataba na klabu ya Bruges ambapo atakuwa akipokea malipo ya £65,000 kwa wiki wakati akiwa anasubiri usajili wake huo uweze kukaa sawa katika klabu yake hiyo mpya.
Kama Manchester United wataridhia kufanya biashara ni rahisi kumuona Fred akiwa Italia kwa mkopo. Klabu ya Fiorentina inaonekana kutaka kumnunua nyota huyo ambaye hadi sasa hajapata wakati wa kubadilishana mawazo hata uwanjani tu akiwa na kikosi fulani. Hivyo, kama ofa hiyo itakuwa na faida kwa United na wakaridhia basi nyota huyo ataweza kujiunga na klabu hiyo.
Tottenham huenda wakampoteza Eriksen ambaye amekuwa akihusishwa sana na klabu za Manchester United au Real Madrid. Klabu hiyo inahofia kumpoteza nyota huyo kwa kiasi ambacho inaamini ni cha hasara sana kutokana na ubora ambao alikuwanao hapo nyuma. Kutoka kuhitajika kwa pesa nyingi hivi sasa nyota huyo huenda akaja kuuzwa kwa kiwango cha £30m pekee jambo ambalo ni la kushangaza mno!
Nyota aliyekuwa akikipiga na Arsenal ambaye ni raia wa Misri, Mohamed Elney anaangalia hatma yake ndani ya klabu hiyo mara baada ya kupata kibali cha kuondoka klabuni hapo kitokana na mahitaji ya kocha wao huyo. Baadhi ya klabu wakiwemo Bourdeux ya Ufaransa zimtua kuanza kumfukuzia nyota huyo ili kumshawishi ajiunge na klabu yao.

