Ligi Kuu ya Italia imeendelea kwa mchezo ambao ulikuwa ukisubiriwa na wengi kutokana na usajili ambao klabu hizo mbili za jiji la Italia zilioufanya. Wengi walikuwa wakisubiri kuona nini kitatokea katika mechi ambayo kwa hakika ilikuwa na piga nikupige ya aina yake katika usiku uliokuwa wa kihistoria sana.
Ndani ya mechi ya Juve na Napoli kulishuhudiwa ufundi wa kila aina huku Juventus wakifanikiwa kuwazidi mbinu Napoli ambao ni wababe wenzao kwenye ligi hiyo ya Italia. Ndani ya mechi hiyo kulishuhudiwa Ronaldo akiendeleza mkanda wake ulioishia msimu uliopita kwa kufunga goli lililoongeza kitu ndani ya ushindi huo.
Klabu zote mbili zimeanza ligi kwa ushindi mkubwa sana na huu ulikuwa ni sehemu ya muendelezo wa wao kufanya vizuri uwanjani kutokana na uwezo wa kila mmoja. Hivyo aliyekuwa anashinda mechi hiyo alikuwa na muendelezo mzuri wa kugawa dozi mara baada ya kufanikiwa kuchukua alama mwanzoni.
Hadi dakika ya 62 Juventus walikuwa mbele kwa magoli matatu ambapo msumari wa Ronaldo uliweza kuonekana kama unawafanya Juventus kuondoka na ushindi huo wa goli hizo 3-0. Lakini, wanasema katika soka lolote linawezekana pale ambapo Napoli waliweza kusawazisha magoli yote matatu!
Baada ya kusawazisha magoli hayo hadi dakika ya 90 ubao ulikuwa unasoma 3-3 jambo ambalo liliona kama mechi hiyo ingeenda kuisha kwa sare ya aina yake lakini mambo hayakwenda hivyo ndani ya ardhi hiyo ya Turin ambapo Juventus ilikuwa ni vigumu sana kwake kuweza kukubaliana na aina hiyo ya matokeo.
Baada ya muda mfupi tu huku mechi ikiwa inaelekea kuisha Juventus wakiwa na ari yao ya miaka yote ya kutokukubali matokeo waliweza kupiga shambulizi ambalo liliwafanya walinzi kuweza kukorogana na kuwaruhusu Juventus kupata goli la kuongoza na kuwafanya kuondoka na alama zote tatu mbele ya mashabiki wake.
Juventus walipata goli lao kupitia kwa Koulbaly ambaye alishindwa kuokoa mpira na kusababisha kujifunga upande wake. Jambo ambalo liliweza kumuondoa kabisa mchezoni kwa sekunde chache zilizobakia mara baada ya makosa aliyoyafanya kwa dakika chache ambapo Napoli waliondoka vichwa chini.


Ally mohamedi ally
Habadiliki huyu fundi