Kocha anayeifundisha klabu ya Barcelona kwa sasa, Valverde alikuwa na matokeo ambayo hayaradhishi kabisa ndani ya kikosi hicho, jambo ambalo likamfanya akae kwenye vichwa vingi vya kuzunguzimiwa kwamba maisha yake ndani ya kikosi hicho huenda yakawa hayana kipindi kirefu zaidi klabuni hapo.
Kikosi hicho cha Barcelona kilishindwa kabisa kuwika katika michuano yake ya hapa karibuni jambo ambalo kwa hakika linaweza kuhatarisha kibarua cha kocha huyo kuendelea kusalia katika klabu hiyo ambayo kwa hakika ni kati ya vilabu vyenye historia ya kipekee sana ndani ya soka.
Wikiendi iliyopita kikosi hicho kilipokea kipigo nyeti kutoka kwa klabu ya Levante kwenye mechi yao ya ligi jambo ambalo liliibua maswali ya pekee sana juu ya mwenendo wa kikosi hicho na hali halisi ya upatikanaji wa matokeo ambapo kikosi hicho kimekuwa kikisuasua kwa namna fulani.
Baada ya matokeo hayo kocha huyo amewwza kuzungumza kwamba hana wasiwasi kwa taarifa zinazomhusisha yeye na kuondoka klabuni hapo kutokana na mwenendo wa matokeo ya kikosi chake. Anachokizungumzia na kukiona zaidi ni kipindi tu ambacho kikosi hicho wanapitia na ana hakika kitabadilika.
Barcelona wapo kileleni mwa ligi hiyo baada ya michezo yao 11 lakini pamoja na kwamba wapo juu ya jedwali hilo hawajawa kwenye nafasi nzuri ya kiushindani kwa sababu hawana alama zinazoweza kuwapa ahueni ya wao kuweza kuitwa ile Barcelona ya ushindani ambayo kila mmoja anawiwa kuiona.
Hapo awali kabla ya msimu huu kuanza aliweza kuzungumziwa kwamba angeweza kuondoshwa klabuni hapo lakini taarifa zinadai kwamba aliweza kukingiwa kifua na Raisi wa klabu hiyo Bartomeo ili aendelee kukaa kikosini hapo na kwamba wampe muda zaidi wa kuweza kupima mwenendo wake.
Zaidi ya hilo aliweza kutoa sare ya bila kufungana kwenye michuano ya klabu bingwa, lakini yeye anadai kwamba hahusiki kwa namna yoyote na matokeo hayo yanayopatikana ndani ya kikosi hicho. Na zaidi akadai hali hiyo ni matokeo ya kawaida sana japo yanahitaji kubadilishwa.
Kabla ya mechi za mapumziko ya kimataifa watatakiwa kucheza mchezo wao dhidi ya Celta Vigo katika mchezo wao wa ligi kabla ya kuelekea kwenye michuano ya kimataifa kwa vaadhi ya nyota walioitwa kuwa sehemu ya vikosi vyao.


Zeiyana
Kwa matokea waliyokua nayo Barcelona si mazuri kwa clabu kubwa kama ile ni vizuri tu wangeangalia upande mwengine inaweza kuwa ndio mwanzo wa mafanikio yao