Bayern Yaongeza Mkataba wa Kocha Wake Mpaka 2023

Klabu ya Bayern Munich inamthibitishia Hansi Flick kama kochaa wake mkuu baada ya makubaliano ya dili la miaka mitatu. Ikumbukwe Flick alipokea mikoba kutoka kwa Niko Kovac kama meneja wa mpito mwezi Novemba, kabla ya Bayern leo kutangaza kuwa amesaini mkataba wa miaka mitatu kuendelea na miamba hiyo ya soka la Ujerumani. Flick mwenye umri wa miaka 55 atatumikia Bayern mpaka mwezi june 2023.

“Timu ina furahia kazi ya Flick “ Amesema mwenye kiti wa timu ya Bayern Karl-Heiz Rummenigge. “ Timu imefanya vizuri chini yake na imecheza mpira wa kuvutia ambao umeleta matokeo mazuri”

“Natarajia kutimiza majukumu yangu ipasavyo nikiwa na wafanya kazi wengine wa benchi la ufundi” Flick aliongezea kwa kusema “mazungumzo yangu na Rummenige, Oliver Kahn na Hasan Salihamidzic yamekwenda vizuri na tuna malengo yanayofanana na tuna aminiana. Kwapamoja tuta onesha  dira na nina hakika tutatimiza vingi pamoja”

Hansi Flick kulia akiwa na mwenye kiti wa Bayern munic Karl Rummenigge

Tangu achukue mikoba ya ukocha toka kwa Kovac, Flick ameipa Bayern ushindi mara 18 katika mechi zake 21 za kupigania kutetea ubingwa wa ligi kuu nchini Ujerumani na kuhakikisha timu hiyo inashika usukani katika msimu wa mwaka 2019-20 wakiwazidi alama 4 wapinzani wao wanao wakaribia kwa ukaribu Dortmund.

Flick pia ameisimamia Bayern kwenye michezo ya robo fainali akiongoza upande wake baada ya kuichapa Chelsea mabao matatu kwa sifuri 3-0 kabla michezo hiyo haija ahiorishwa kutokana na janga la Korona (Covid19).

Kwa Flick hii inakua mara yake ya kwanza kua kocha mkuu tangu alipopata nafasi hiyo akiwa na Hoffenheim mwaka 2005. Tangu hapo amekua akihudumu kama kocha msaidizi kwa timu ya taifa ya Ujerumani kabla ya kua msaidi wa Kovac kwa msimu wa mwaka 2019-20.

4 Komentara

    Hongera kwa frick kusaini mkataba

    Jibu

    Hongera sana.

    Jibu

    Bayern lazima waongeze mkataba

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.