Straika wa Simba SC, Meddie Kagere amewasema mashabiki wa Kenya kawa kutokuzipenda timu zao kama ilivyo kwa Tanzania.
Kagere, ambaye amecheza nchi nne katika klabu tofauti ukanda huu, ikiwemo Uganda, Rwanda, Kenya na kwasasa Tanzania, anaamini mashabiki wakipenda timu zao wanaweza kuzifuata timu zao hata vijijini kutazama wakicheza wakati wakenya hawafanyi hivyo timu zao zikicheza.

“Mashabiki wa Tanzania wanapenda timu zao na mpira,” amesema Kagere.
“Hawakosi mchezo hata kama unachezwa vijijini watakwenda kutazama, lakini ni tofauti na Kenya kwani wakati mwingine unacheza uwanja ukiwa mtupu na mashabiki wengine hawajui kama hata mpira unachezwa.”
Kagere, ambaye amechezea Gor Mahia akiwa kwenye kiwango bora na ameshinda Ligi Kuu mara mbili KPL, amesema walikuwa wana uhakika wakushinda mechi zote kwa sababu kulikuwa hakuna upinzani.

“Hakuna upinzani ukienda Kenya. Kuna timu moja tu na ni Gor Mahia,” Kagere ameongezea . “Wakati nipo kule nilicheza nikijua tunashinda taji. Tulienda kucheza tukiwa na uhakika tunaenda kushinda.”
“Ushauri wangu kwa wachezaji wa Rwanda lazima ujipe changamoto wenyewe kama unahitaji kitu. Nilianza chini, Nimetokea Atraco siku fanya kazi na nmeanza upya, kisha Kiyovu, Mukura, na Police FC. Kuna changamoto nyingi lakini nilisema, nataka nifike mahali” Alisema Kagere
Striker huyo alimaliza msimu uliyipita na magoli 23 na kusaidia timu yake kunyakua Ubingwa.


Issa
Ndio wabongo mpira ndio asili yetu sana