LAZIMA NITANYAKUA MEDALI YA OLIMPIKI -  Frazer Clarke

Mwana masumbwi Frazer Clarke anajiandaa kua bingwa mwingine wa Dunia wa uzito wa juu kutoka Uingeleza kwenye mashindano ya Olimpiki, Lakini wa uzoefu juko nyuma sana kulinganisha na Antony Joshua. Kama ilivyo kwa wengi Clarke anatakiwa kusubiri mwaka mmoja Zaidi, Lakini wapenda masumbwi wanasema Clarke amesubiri kwa Zaidi ya miaka 10.

“nimekua na timu ya taifa kwa Zaidi ya miaka 10, tangu mwaka 2009 na bado sijatambulika, na nikiangalia na huu utaratibu wa kufungia michezo ndo nazidi kuoana uwezekano unachelewa’’ Clarke akiongea na Skysport

Frazer Clarke wa pili Kushoto mwenye sweta jekundu

“nimesubiri kwa Zaidi ya miaka 10 sasa na nimekua nikijiambia kua ni mwaka ujao tu umebaki, ila kinachotokea nasubiri tena mwaka mwingine, nilibakiza siku chache tu nishiriki Olimpiki lakini Mambo yamebadirika na natakiwa tena kusubiri mwaka mwingine.”

Tangu Olimpiki izuiliwe Clarke amesema na kukubali kua Afya ina umuhimu Zaidi kuliko masumbwi hususan kwenye kipindi hiki cha Virusi vya Korona (Covid19)

Lakini bado kama mashindano hayo ya Olimpiki yataendelea kufanyika Jijini Tokyo Japan hapo mwakani mwana masumbwi Clarke atakua na miaka 29 kipindi cha majira ya joto mwaka huu na lengo la kuvaa medali ya Dhahabu baado litakua lipo pale pale.

Mpango wa Clarke ni kupigana kwenye olimpiki na kuchukua medali kipindi cha majira ya joto hapo mwaka 2021 na Clarke kwa muda huo atakua na miaka 30, Joice alikua na umri huohuo wakati ana chukua medali yake ya Silva mwaka 2016, kwa hiyo kwake ndoto haiwezi kuzimika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.