Golikipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois amethibitisha kuungana na mastaa wengine wa F1 kwa ajili ya michuano ya kidigitali kwa mtanda ya mbio za magari.
Mpaka sasa Courtois, Leclerc & Norris tayari wameshasthibistisha ushiriki wao wa michuano hii ambayo imeanza kushika hatamu siku za hivi karibuni kama mbadala wa mbio za magari za kawaidia ambazo zimesimama ili kuepusha misongamano.
Staa huyu wataungana na madereva wa Formular 1 kuchuana kwenye mbio za magari za mtandaoni zikifahamika Virtual F1 Esports. Golikipa huyu wa Real Madrid watachuana pamoja na maastaa wengine wakiwemo Charles Leclerc na Lando Norris kwa Jumapili. Michuano hii ya mtandao itatumia mandhari ya china.
Leclerc takuwa na wenzie watano kutoka F1 2020 ambao Alex Albon, Lando Norris, Antonio Giovinazzi, George Russell na Nicholas Latifi wataingia mchezoni mubashara Jumapili.
Thibaut Courtois anasema mabingwa wa mbio hizo kwa mtandao tayari wameshamfundisha baadhi ya mbinu na amekuwa akijiandaa kwa kipindi fulani sasa, anatarajia kufanya vyema kwenye michuano. Majina mengine makubwa ya washiriki bado hayajatangazwa.


Furahav
Habari nzuri.
aisha
Jamaa yuko vizuri