Akiwa ametoka kupasha kwenye michuano ya Hopman Cup kule Perth, Serena alifanikiwa kushinda mechi zake zote tatu akidhihirisha ubora wake toka ajifungue mtoto wake. Wengi walidhania mchezaji huyo maarufu wa tenisi, Serena Williams angelega viwanjani baada ya kuanza jukumu hilo lakini ikawa tofauti na dhana zao.
Serena aliwahakikishia kwamba walichokuwa wanakijenga wao sicho alichokuwa anakiamini yeye kichwani mwake. Kwamba, kuzaa na kulea hakumzuii yeye kufanya makubwa uwanjani zaidi yake ni kujiamini na kufanya mazoezi yanayomfanya yeye kama mchezaji asishuke kwenye kiwango chake.
Sasa akarejea kutoka kulea akarudi uwanjani kwa kasi kujaribu kupigania nafasi yake akiwa katika ubora wa aina yake. Alirudi katika michuano mikubwa ya Australia Open, kocha wake akiamini kwamba ni wakati pekee wa Serena kufanya makubwa kutokana na wakati aliopitia huko nyuma na kukosa kushiriki michuano mikubwa mingi iliyopita.
Kocha huyo amemuongoza mchezaji huyo katika michuano 10 kati ya 23 ambayo imechezwa na mwanadada huyo. Imani yake na nia yake ni kumfanya Serena bora zaidi na aweze kuibuka mshindi katika mashindano anayoshiriki kwa wakati huu kutokana na kuanza kurudi katika ubora wake ni suala ambalo linaleta matumaini kwake hadi sasa.
Serena kitabibu bado anaendelea kujijenga ili aweze kurejea kwa asilimia zote 100 kama inavyofahamika kibinadamu kulea na kuwa michezoni hasa kwenye michuano mikubwa kama hiyo ni suala linalohitaji kujipa muda wa kutosha na mazoezi mepesi. Alikuwa anahitaji muda wa kutosha aweze kujikusanyia vikombe vingi zaidi kwa wakati ule.
Uwezo wake haukuwa wa kubezwa kabisa, anafahamika kitu gani anakifanya akiwa uwanjani siku zote huwa ni tishio kwa wapinzani wake. Aina ya uchezaji wake ni ya wale wenye uzoefu wa muda wote; mpinzani huhitaji nguvu ya ziada ili aweze kushinda angalau hata seti moja katika michezo yake, kwa sababu ana uwezo wa kumsoma mpinzani haraka na kutafuta matokeo wakati wowote anaohitaji.
Ni suala la muda tu kwake kuweza kurudi kuijenga historia yake aliyoiacha kwa kipindi kirefu sasa. Alirudi uwanjani akiwa na njaa kubwa ya kutaka kuudhihirishia ulimwengu kwamba umri wake, kulea na afya yake vimerejea kwenye ubora wake tofauti na wengi wanavyomuwekea wasiwasi kwamba anaweza kuwa na wakati mgumu kushiriki kwenye michuano hiyo. Kwake suala ni moja tu kurejesha heshima na mataji ili aendelee kujenga historia katika mchezo wake wa tenisi.
Hakika atafanya makubwa sana katika michuano hiyo mikubwa kama ile ya Australia Open.


devotha
hongera sana Sellena