Ferenc Puskas and Alfredo Di Stefano (Real Madrid), hawa ndio historia ya Madrid ya sasa kwa makubwa waliyoyafanya miaka ya 1950 hadi 1960, waliponyanyua ndoo ya klabu bingwa mara tano ndani ya miaka hiyo. Pamoja na muunganiko wa Ronaldo, Bale na Benzema kuonekana ulikuwa imara; lakini wawili hawa waliandika historia kubwa ya kuwaweka Los Blancos kwenye ramani ya kufahamika na kuwa klabu kubwa sana duniani. Muunganiko wa wachezaji hao ulifunga mabao 360 katika mechi 433 walizocheza pamoja; huku Di Stefano alifunga magoli 156 katika mechi zake 229: wakati Puskas akifunga 193 katika mechi 227 alizocheza. Hadi sasa bado wapo kwenye takwimu za wachezaji waliofunga magoli mengi kwenye klabu hiyo.
Wayne Rooney and Cristiano Ronaldo (Manchester United), baada ya kutua kwa Mourinho katika ligi ya Uingereza kulionekana kama ni tishio kwa Man united kutokana na kuondoka kwa wachezaji tegemezi wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Wachezaji kama David Beckham, Rudd Van Nistelrooy na Roy Keane waliweza kustaafu soka la ushindani katika klabu hiyo na kuonekana inaweza kuwa ni wakati wa Mreno huyo kufanya makubwa klabuni hapo. Lakini mambo yalikuwa tofauti katika timu ile baada ya uwepo wa muunganiko wa wachezaji hawa wawili waliojenga historia iliyoachwa na watangulizi wao. Japo hawakudumu sana na miaka ya 2004-2009 waliweza kutawanyika.
Thierry Henry and Dennis Bergkamp (Arsenal), baada ya Wenger kuichukua timu hiyo miaka ya 1996 alikuwa na jukumu la kuhakikisha anavunja uteja wa kupokea vipigo kutoka kwa Ferguson ambaye kwa wakati huo alikuwa ni tishio katika ligi hiyo kitu ambacho kiliwatisha wengi miaka hiyo. Pamoja na kukijenga kikosi hicho alifanikiwa kuweka vizuri safu yake ya ushambuliaji baada ya kumsajili Henry aliyekuwa Juventus kwa wakati ule wa miaka ya 1999. Muunganiko wa wawili hawa ulikuja kuzaa vitu vya pekee ndani ya klabu hiyo kitu ambacho kilikosekana kwa kipindi kirefu.
John Toshack and Kevin Keegan (Liverpool), katika miaka ya 1970 majogoo hawq walikuwa ni miongoni mwa klabu zenye mafanikio makubwa sana. Hii ilichangiwa na nguvu kazi ya washambuliaji hawa ambao katika muunganiko wao walifanya kila linalowezekana ili kuipa ushindi timu hiyo. Wakiwa pamoja walifanikiwa kufunga magoli 189 katika michezo 522, hii ikiwa ni miaka ya 1971 hadi 1977 tu.
Romario and Hristo Stoichkov (Barcelona), klabu hii imebahatika kuwa na wachezaji hatari kama Xavi, Iniesta na Messi pia muunganiko mwingine wa Messi, Suarez na Neymar; lakini hawawezi kufikia kazi kubwa iliyofanywa na watu kama hao wawili ambao walikuwa sio kitu cha mchezo wanapolifikia lango la mpinzani. Romario alijiunga na miamba hao miaka ya 1993 lakini alimkuta klabuni hapo mkongwe wake Stoichkov ambaye alikuwepo klabuni hapo tangu miaka ya 1990.


Furahav
Asante kwa habari.