Robben- Ferguson Akanunue Jezi Yangu, Kabla ya Kunisajili

Achana na Roben wa fainali ya UEFA pale Wembley, Dortmund wale warahisi tu. Achana na Maajabu ya kupigwa buti na timu nzima pale Allianz Arena, St. Pauli wale watoto tu. Achana na perfomance yake ile nusu fainali ya UEFA, Barcelona hawajui kukaba wale. Mzungumzie Robben dhidi ya wa Hispaniola pale Brazil bwana.

Ukuta wa Hispania usiku ule, Ceaser Azplicueta, Gerad Pique, Sergio Ramos na Jordi Alba, aliuchana peke yake. Iker Casillas na miaka yake 16 kwenye ugolikipa, Robben hakujalisha. Alimrudisha utotoni, akamwambia tambaa kaka mkubwa njoo. Mabeki wakaamua kuwahi golini walinusuru lango lao. Kwa ukatili Robben akapiga kwenye nyavu ndogo kupitia kwenye post, ili wasizuie.

Arjen Robben


Waulize waholanzi utoto wake pale nyumbani PSV Eindenhoven. Wakati wanamuita Denis Berkgamp “the non flying dutchman” wakamtofautisha Roben kwa kumuita “the flying dutchman”. Walimpa tuzo ya mchezaji bora wa msimu akicheza pembeni ya Mateja Kezman. Ile patnership hawajaisahau mpaka leo wanaiita “Robben and the batman”

Alipanda ndege kwenda Manchester kuzungumza na Ferguson, Fergie aliweka mezani euro million saba, dau ambalo PSV waliona ni matusi. Mwenyekiti wa PSV Hary Van Raij alimwambia Fergie hilo dau anunulie jezi ya Roben😀. Tajiri Roman Abramovich alilipa euro 18 million, akajiunga na Chelsea.

Alirudi Old Trafford April 7 2010 kumkumbusha babu kosa alilofanya kutokumsajili. Alikuwa kitanzi cha man utd usiku ule. Mpira wake aliouunganisha mojamoja (volley)ulijaa kambani na kuivusha Beyern Munich kwenda nusu fainali ya Champions league. Bao la kigaidi lile.

Tunamjua kuanzia kwenye playstation🤗, anacheza winga ya kulia ila anatumia mguu wa kushoto. Akipata mpira unamuingiza ndani kwa kuja katikati, akiingia ndani ya box unapiga shuti, anafunga. Uhalisia wake uwanjani ulikuwa hivohivo. Mabeki wanajua atakachofanya ila hawawezi kumzuia.

Imeandaliwa na @deo_mwanasoka

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.