Mabingwa wa China Guangzhou Evergrande siku ya Alhamisi ya April 14 wameanza kujenga uwanja mpya utakao gharimu dola bilioni 1.7 (Tsh. Trilioni 3.9) na utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 100,000.
Uwanja huo utakuwa moja ya uwanja wa soka mkubwa zaidi duniani, na umetarajiwa kukamilika ifikapo 2022.

Wazo nyuma ya muonekano, ni shepu ya ua la lotus, ambalo linapatikana Guangzhou ndio maana linajulikana kama ‘jiji la maua’.
Raisi Xia Haijun, wa Evergrande, wamewaambia waandishi kwenye sherehe ya ufunguzi wa ujenzi wa uwanja mpya “Uwanja wa Evergrande utakuwa moja ya uwanja bora Duniani ukifananishwa na Sydney Opera House na Burj Khalifa wa Dubai, na utakuwa alama muhimu kwa mpira wa miguu China kwa Dunia.”


Povel
Duh
Issa
Safi sana china