Msimu wa Ligi kuu nchini Uholanzi maarufu kama Eredivisie kimsingi umekwisha, kufuatia tamko la waziri wa nchi kupiga marufuku michezo hadi mwezi Septemba.
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Uholanzi (KNVB) limesema linatarajia kumaliza msimu wa Eredivisie wa 2019-20 baada ya waziri mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte kutangaza Jumanne kuwa Michezo yote ni marufuku hadi Septemba 1 kutokana na janga la virusi vya Corona.

Ligi Kuu ya Uholanzi imesimamishwa tangu mwezi Machi, ikiwa na michezo tisa iliyobaki kumaliza msimu na Ajax ndio anaongoza msimamo mbele ya AZ kwa tofauti ya magoli.

Ingawa ligi nyingi barani Ulaya zinafikiria kurudi mwezi Juni na michezo kufanyika bila mashabiki, Rutte amesema kwamba hata mechi zikiwa hazina mashabiki haziruhusiwa hadi mwanzoni mwa mwezi Septemba.
Kufuatia tangazo la Rutte, KNVB imetoa taarifa ikisema inatarajia kumaliza msimu wa Eredivisie na itawasiliana na UEFA ili kujua utaratibu wa kumaliza msimu.
Matokeo ya msimu mzima yanaweza kufutwa, au KNVB inaweza kuamua kumpa Ajax ubingwa kulingana na msimamo wao wa sasa wa Eredivisie


felister
safi
isha
Big up
Issa
Mmh tutakosa raha dah
Gabriel
Habar njema sana 👍
Nasra
Gud news