Mario Gotze Fundi wa Kijerumani Anaehusudu Soka la Kujituma

Katika ile Borrusia Dortmund iliyochukua Bundersliga back to back kulikua na watu sana , Klopp alikusanya vijana wengi wazuri na wenye vipaji vya kutisha na moja yao alikuwemo Mario Gotze . Yes pengine alikua anahesabika kama mafundi sanaa mwaka huo , lazima uwepo mpango kazi wa kumzuia ni lazima iwe ivyo . Maisha yake pale Dortmund yalikua kama mwanga mkali ndani ya giza , alikua kama mfalme ndani ya ngome , pengine alikua ndo mtu muhimu zaidii katika mfumo wa Klopp…

Gotze na Klopp

Tunamzungumzia Mario Gotze kiungo mshambuliaji wa zamani wa Borussia Dortmund , Buyern Munich na sasa amerudi Dortmund . Gotze ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi zozote katika kushambulia , kwanza ana uwezo wa kucheza kama kiungo mshambuliaji , pili ana uwezo mkubwa wa kucheza kama mshambuliaji pacha katika 4-4-2 , tatu ana uwezo mkubwa wa kutokea upande wa kushoto katika kushambulia ile Dortmund iliteleza asilimia kubwa katika 4-2-3-1 au 4-3-3 . Katika Gengeng pressing ile ya Klopp pale Dortmund alifana aina zote mbili muhimu kwanza kabisa Open Play au Counter Attacks

Mario Gotze

Jurgen Klopp alimchukua moja kwa moja kutoka timu ya vijana aliona kuna madini pale , beki na kiungo wa zamani wa Ujerumani Franz Anton Beckenbauer alimwita kama Messi wa ujerumani , uwezo wake mkubwa wa kukokota mpira , chenga , uwezo mkubwa wa kufunga , kasi na ubunifu wa hali ya juu hakika alikua kijana hatari sanaa . Aliondoka Borrusia Dortmund mwaka 2003 kujiunga na mahasimu wao Buyern Munich , alikwenda kufungua ukurasa mpya kimpira kifupi aliamua kwenda duniani na alivuruga kabisa mipango ya Klopp kama alivofanya Phillipe Coutinho pale Liverpool , yaani aliondoka muda ambao Dortmund walimuhitaji zaidi kuliko alivoiihitaji yeye.

Mwaka 2013 akiwa na miaka 21 aliamua kwenda kuungana na kocha wake kipenzi Pep Guardiola alipenda sana kufanya kazi chini ya Pep . katika misimu yake miwili ya kwanza alionesha mwanga mkubwa hasa pale mwaka 2014 alipojumuishwa katika wachezaji 23 wanaogombea Ballon D’or , licha ya kuonekana kama totobad wa baadae bado malegend kadhaa waliendelea kumponda na kumkandia kwa kua na performance mbovu . Pale Buyern Munich hakuiona heshima kama ya pale Dortmund , hakuonekana kufanya la maana alionekana kama mbabaishaji tu na utoto mwingi .Baada ya miaka mitatu alirudi kundini yaani alirudi Dortmund na alinukuliwa akisema anajuta kuihama klabu hiyo.

Pale Dortmund hakua mfalme tena akawa kama mfanyakazi tu , tayari fundi Marco Reus alishachukua kiti chake muda wote kuanzia mazoezini hadi kwenye mechi alihesabika Marco kama ndio mfalme , licha ya kwamba Reus alisumbuliwa sanaa na majeraha lakini mashabiki wapo nae bega kwa bega , Piere Aubemeyang alikua star lakini Reus alikua mfalme .Hakukua na hakuna dalili za Mario Gotze kua mfalme tena pale , wanamchukulia kawaida sanaa na hawana habari nae . Kibaya Dortmund kila kukicha wanaleta mafundi wa mpira kama kina Sancho , Halaad , Hakimi , Thorgan Hazard , Julian Brandt na wengine wengi.

Dortmund hawana malengo tena na Mario Gotze amewekwa sokoni , hakuna kocha mkubwa anayeonekana kumtaka . Watu wameshamsahau kabisa yaani amesahaulika , ufundi wake hauna manufaa kwao , lakini ataendelea kua vichwani mwa wajerumani kwani aliwafungia goli la ushindi dhidi ya Argentina katika fainali ya kombe la dunia . Pengine hana presha sanaa ni motto wa kishua huyu , baba yake ni professor katika chuo cha Dortmund University of Technology hana shida ataendelea kula maisha na mrembo wake Ann-Kathrin Brommel…

3 Komentara

    Good article

    Jibu

    Makala nzuri

    Jibu

    Gotze duh streika hafai

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.