Akiwa na miaka 25 tu, alishashinda Champions league 4, la liga 2, world cup 1 na jumla ya makombe 16. Hayo ni mafanikio zaidi ya legends kama John Terry, Steven Gerrard na Wayne Rooney. Bahati iliyoje kucheza Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa zote zikiwa katika ubora wake.

Historia yake inaanza pale Lens, Ufaransa. Walimtaka achezee under-17, under-19 na timu ya wakubwa. Zote kwa pamoja . Tatizo la kuwa bora kwenye timu mbovu ukiwa na umri mdogo. Walimpa kitambaa cha unahodha akiwa na miaka 17 tu. Alisaini mkataba wa kudumu nao hadi 2015, ila waliposhuka daraja akasepa zake. Nani akacheze mchangani wewe.
Kipindi kile anatambulishwa Real Madrid akiwa na jezi 19 mwaka 2011, watu pale Santiago Bernabeu wanamuhuria. Huyu mtoto anakuja kucheza nafasi ya nani sasa? Pepe, Ramos au Ricardo Carvalho. Anacheza nafasi ya nani kwa hao binadamu. Laiti kama wangejua bwana mdogo anamletea Mourinho ugomvi na Pepe, laiti kama wangejua bwana mdogo ameshuka kama malaika wa Gomora na moto wa sodoma, wasingeongea.

Unamkumbuka Varane yupi? Mimi Namkumbuka Varane wa 2014, kwenye ile fainali ya UEFA, baada ya Ronaldo kufunga lile bao la mwisho. Alimpiga Diego Simeone na mpira wakati anashangilia. Kilichofuata? “El Chollo” alipelekwa jukwaani.
Baada ya kucheza dakika zote pale Urusi kwenye world cup, wafaransa walimsamee kosa alilolifanya 2014 pale Brazil. Uzembe wake wa kutokumshika Matt Hummels uliwaondoa kwenye hatua ya robo fainali.


Ester jackson
Ndivyo inavyo takiwa juhudi pekee ndiyo inayoletaafanikio