Kenneth William Bates alizaliwa Disemba 4 1931 ni Mfanyabiashara wa Uingereza aliyejikita kwenye mpira wa miguu na mahoteli. Amehusika kutengeneza Premier League, maendeleo ya uwanja wa Wembley na Mwenyekiti wa zamani wa Chelsea na Leeds United.
Bates alikuwa mwenyekiti wa Oldham Athletic miaka ya 1960 lakini pia aliwahi kutumia Wigani. Mwaka 1982 aliinunua Chelsea kwa £1. Katika kipindi cha umiliki wake ndio aliisaidia Chelsea kulipa madeni na kupambana na wamiliki wa uwanja baada ya kutaka kuwatimua Stamford Bridge. Katika mwisho wa umiliki wake Chelsea walikuwa kwenye nafasi ya top six kwenye EPL.
Ken Bates aliinunua Chelsea kwa £1.00 wakati klabu ikiwa kwenye hali mbaya kiuchumi. deni la klabu lilifikia 1.5million 1982 alikubali kuchukua na madeni yote. Hii ilikuwa baada ya uongozi mbovu wa aliweka majengo ya klabu rehani miaka 1970.

Bates alinunua Chelsea 1982 klabu na sio uwanja, kampuni iliyomiliki uwanja wa Stamford Bridge na klabu ni kampuni mbili tofauti, hii ilikuwa ni kwasababu ya deni ya klabu. Bates alivyoichukua Chelsea alikubali kulipa pesa kwaajili ya kutumia uwanja wa Stamford Bridge.
Mears ndio alikuwa anamiliki hisa nyingi katika SB Properties, tulikubaliana kuungana ili kununua hisa za Mears kwenye SB Properties kwa £450,000. Bates, baadae niligundua kuwa Mears alikuwa na mazungumzo na mmiliki wa Crystal Palace Ron Noades akiwa na lengo la kuihamisha Chelsea kwenda Selhurst Park. Lakini baadae Mears na Lord Chelsea waliuza hisao zao za SB Properties 70% kwa Marler Estates, Marler akaanza kampeni ya kuitimua Chelsea, ili Stamford Bridge uendelezwe.
Hali iliendelea kuwa mbaya hadi Bates alipoamua kununua hisa chache za SB Properties na kuanzisha kampeni ya kuunusuru uwanja iliyoitwa “Save the Bridge” yenye lengo la kuchangisha £15 million ili kununua hisa zote za SB Properties.
Baada ya kuvutana sana, Chelsea walipewa taarifa ya kuondoka Stamford Bridge. Mwaka 1989 Marler alifilisika na ndipo Bates alipoifiata Benki kuomba mkopo ili kunusuru uwanja usiuzwe tena kwa mtu mwingine. Bates alianzisha Chelsea Pitch Owners ambayo ni taasisi isiyo na faida itakayomilikiwa na mashabiki, wakaununua uwanja na haki za jina la klabu ilikuhakikisha hakuna waendelezaji wowote watakaonunua uwanja Stamford Bridge.
Ilikuwa mwaka 2003 ndio Bates alifikia makubaliano ya na Bilionea wa Urusi Roman Abramovich kununua zaidi ya 50% ya klabu kama kampuni mama.
Bates alikuwa akimiliki 29% ya hisa na wengine ambao walikuwa wakimiliki hisa zao walikuwa tayari kuuza hisa zao kwa Bilionea wa Kirusi.

Abramovich aliinunua Chelsea kwa £140million Julai 2003 kutoka kwa Ken Bates. Baada ya Roman kuinunua Chelsea alitumia £121m kwenye dirisha la kwanza kipindi cha kiangazi kama Damien Duff, Hernan Crespo, Claude Makelele na Juan Sebastian Veron na timu ilimaliza nafasi ya pili chini ya Claudio Ranieri.


Furahav
Boc kubwa hilo.
isha
Duuh huyu jamaa kumbe ni boss ivi