Sote tunafahamu bondia Mike Tyson aliamua kustaafu rasmi mwaka 2005. Tangia hapo bingwa huyu hajapigana ndondi za kulipwa mpaka sasa. Lakini Tyson anataka sasa kurejea Ulingoni.
Licha ya kustaafu, Mike Tyson aliendelea kupeta kwenye tasnia ya filamu akishirikiana na waigizaji wengi wakubwa duniani. Hivi karibuni akiweka wazi nia yake ya kurejea ulingoni amesema tayari anafanya mazoezi kujiweka fiti.
Mike Tyson amekuwa akifanya mazoezi hayo kuelekea shindano linaloweza kuandaliwa kwa ajili ya maonesho ya ndondi ili kukusanya pesa za kusaidia jamii.
Bondia huyu mwenye miaka 53 sasa, ana rekodi ya matumizi ya madawa, usumbufu wa kutumia madawa ulitua kwa nyota huyu.
Akizungumza na TI kupitia ukurasa wake wa Instagram, alisema kuwa anajinoa vilivyo kurejea
“Mwili wangu umechangamka sana, na maumivu ya kupiga mitt. Nimekuwa nikifanya mazoezi, nimekuwa nikijaribu kutafuta maonesho ya ndondi. Nitarejea kwenye fomu na nitaweza kupigana kama raundi 3 au 4 kwa ajili ya kukusanya pesa za msaada” -Mike Tyson

Mike Tyson aliaamua kustaafu baada ya kupambana dhidi ya Kevin McBride na kushindwa kuendelea katika raundi na raundi ya 7 licha ya kuongoza kwa pointi hadi raudni ya 6. Aliona ulikuwa ni wakati muafaka yeye kustaafu baada ya kutawala ndondi kwa mda mrefu.


Daniel
Mike Tyson is one of the greatest
Sylvester
He is the one of the boxing legend
Furahav
Bingwa wa dunia.
Adelta
Dunia mzima inamtambuwa
Tumpe hongera zake