Ndoto ya Zidane Kupata Warithi wa Ronaldo, Bale na Benzema

Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane anataka kutimiza ndoto yake ya kupata warithi wa nafasi tatu klabuni hapo. Zidane anataka kupata warithi wa Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema.

Katikia ndoto zake, Zidane anataka safu yake ya mashambulizi kuwa na Kylian Mbappe, Erling Halaand na Eden Hazard mpaka kufikia msimu wa joto wa 2021.

Wakuu wa Real Madrid wametajwa kuwa wanapania taratibu kumnasa Mbappe na Haaland, ikiwa ni ndoto ya Zidane kuwa na safu ya watatu hao baada ya kufanikiwa kumsajili Eden Hazard msimu wa joto uliopita.

Inakaaje hii? Mbape akiweka kambi kulia, Hazard akatia kambi kushoto, katikati tumshuhudie Haaland akidua hapo! Kwa mujibu wa chapisho la AS, Zidane anaamini itakuwa burudani sana kwenye mashambulizi.

Matumaini ya Zidane ni kuwa watatu hawa watakuwa na ladha ya watata watatu ambao ni Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema walivyokuwa wanaendesha mashambulizi.

Tangia kuondoka kwa Ronaldo, Real Madrid wanatajwa kuwa bado hawajapata ladha ile ile ya Ronaldo katika safu ya ushambuliaji. Itachukua mda kufanya hivyo. Ni matumaini ya Zidane kuwa watatu hawa watafaa zaidi kubadilisha utamu wa soka pale Real.

Hata hivyo kazi bado ipo kunasa sahihi za mastaa hawa! Wakati PSG wakiwa hawana mpango wa kumuachia Mbappe, Liverpool nao wamekuwa wakihusishwa naye. Man United wamekuwa wakihusishwa pia na Haaland. Real wakiweza kuruka viunzi hivi ndiyo wataweza kuboresha safu ya ushambuliaji ya ndoto za Zidane.

35 Komentara

    mmmh si rahis

    Jibu

    Itachukua muda kutengeneza timu yake.# meridianbettz

    Jibu

    Kwa kizazi hiki hakuna na hatawapata

    Jibu

    Uwenda ikatimia ndoto yake

    Jibu

    Kwa Ranaldo itachukua muda ila Bale na Benzema wanapatikana tu

    Jibu

    itachukua muda sana#meridianbettz

    Jibu

    Mbappe asijiwahishe kwenda madrid tutamsahau …zidane awakuze wakina Assensio tu

    Jibu

    Asante kwa taarifa meridianbet

    Jibu

    Sio rahisi kupata chemistry anayotaka, mara chache hutokea kupata watu sahihi#meridianbettz

    Jibu

    Pengo la Ronald bado mtihan

    Jibu

    Mm sizani kama ndoto itatimia maana cr 7 ni mtu mwingine

    Jibu

    Thanks kwa meridian kwa information

    Jibu

    Huu mchukato mgumu sana nadhani wanahitaji muda kuwapata.

    Jibu

    anaweza kuwapata kwana wenyevipaji wako wengi na wanafanya vzr

    Jibu

    Atapatikana tuu

    Jibu

    Zidane huwa hakosei

    Jibu

    Itachukua muda sana

    Jibu

    mara chache hutokea kupata watu sahihi#meridianbettz

    Jibu

    Itachukua muda kupata MTU kama CR7

    Jibu

    Duh bado sana

    Jibu

    Sio kirahisi kama wanavyofikiria

    Jibu

    Sio rahis wanavyofikilia

    Jibu

    Ni rahisi kama hao anaopambania wawe na nia ya kweli na kujituma kwa uhakika ndipo ndoto zake zitatimia

    Jibu

    Siyorahisi kumpata mtu km Cr7

    Jibu

    Kupata kama wao na muunganiko wao sio rahis

    Jibu

    Kuwapata Kama wale Tena ni kazi kubwa sana

    Jibu

    Axante kwa taarifa

    Jibu

    Good newz

    Jibu

    Mmh sio rahisi kama anavyo zani lakin ajaribu labda wanaweza tokea

    Jibu

    Mmmh sidhani kama atafanikiwa

    Jibu

    Mmmh itskuwa hatar sana.

    Jibu

    Ahsant kwa taarifa#meridianbeti

    Jibu

    hii itakua vizuri japo ni kazi ngumu kwake

    Jibu

    Ahsante kwa taarifa

    Jibu

    Ahsanteni kwa taarifa nzuri za kimichezo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.