Jose Mourinho alipotimuliwa klabu ya Manchester United, alilazimika kukaa kwa mda fulani kabla ya kupata kibarua chake kipya. Wakati akitarajia kupata kibarua kipya alisema kwa wakati ule alikuwa anajiona kazi yake inayofuata ni kwenye timu ya taifa.
Mapema tu baada ya kutimuliwa, klabu kadhaa ziliripotiwa kumuhitaji kama meneja. Mourinho alinukuliwa akisema wazi kuwa kuna klabu ambazo tayari zilishamfuata lakini aliamua kukataa akiamini sio aina ya kazi aliyohitaji au klabu alizotaka kuwepo kwa wakati huo.
Moja ya klabu alizokuwa akihusishwa nazo ni pamoja na Chelsea, lakini aliamua kutamka hadharani kuwa yeye anajiona katika levo zingine za kufundisha timu ya taifa. Alienda mbali zaidi kwa kusema ni kitu kilichoishi akilini mwake kwa mda mrefu.

Mourinho alinukuliwa akizungumza na Eleven Sports:
“Ninahitaji kupambana katika mashindano mapya. Nafikiria kuhusu Kombe la Dunia na Michuano ya Ulaya.”
“Kwa mda mrefu sasa nimekuwa na hamu ya kujaribu suala hili. kwa sasa, najiona nikiwa kama meneja wa timu ya taifa zaidi kuliko meneja wa klabu.”
Baadaye Mourinho aliteuliwa na Tottenham, Mwishoni mwa Novemba 2029 ambako mpaka sasa ana mipango mikubwa ya kuwarejesha kwenye reli kwa namna yake. Anatarajiwa kuwepo hadi mwaka 2023, Juni. Huenda akafanikiwa zaidi akiwa hapo.
Je ndoto yake imefutika? Huenda, akapata Taifa litakalomuamini kumkabidhi timu ya taifa siku za mbeleni.


mwakalosi
Huyu jose na wakala wake sio watu wa kuwaamini sana wanachoongea
Salma
Wacha tuwe na amani nae yupo huyu jamaa
SADICK
Mourinho amepata mafanikio kwa mbinu zake za kale kwa bahati mbaya kwake mbinu za mpira zimebadilika sana hawezi kupata mafanikio tena kama zamani asipobadilika hata kama atapewa timu ya Taifa ya Ufaransa #meridianbettz
David pere
Mbinu zake zishavuja hawezi kupata mafanikio Kama zamani ,Ndio maana hatapata hata kidogo nafasi ya kufundisha timu ya taifa
Theckla
Mambo yanakwenda yanabadilika
Adelta
Huy kocha anatakiwa kutafuta mbinu
Mpya ya sasa
Dorophina
Kocha yuko vizuri sana labda atafanikiwa
Furahav
Huyu kocha anajua sana.
Antony Luseno
Jose falsafa yake imekaa vizuri katika kuwa kocha wa klabu na sio timu ya taifa
lombo
gud newz asante
Gabriel
Huyu kocha yuko vzur na mzoefu anachoongea anauhakika nacho
Ester
Huyoo jamani apumzike tu hana jipya
Rehema
Huyu Jose ni kocha mzuri sn ananifurahisha sn pole timu yake ikicheza anipa Raha sn
aisha
asikate tamaa ila anatakiwa atafute mbinu mpya
Rehema Dickson
Yuko vizuri sana jose ajipe muda tu kila kitu kitakua sawa
Khadija
huyo kocha yupo vzr sana#meridianbettz
Ernest
Mourinho bado ananafasi ya kufundisha timu ya taifa kutokana na style yake.
felister
Hana mbinu mpya mourihno mm namshauri atulie tu
Juliana
Mourinho ni kocha mkongwe, pia mzuri kwenye kazi yake,but watu wanakuwaga na mashaka mashaka tu
Genia skaluzwe
Huyo kocha mazuri sana
Mwanaidi
Duuuh kazi ipo hapo
Amani
Huenda, akapata Taifa litakalomuamini kumkabidhi timu ya taifa siku za mbeleni.
Lydia Emmanuel Magoti
Mtu asie mkubali Mourinho anamkosea ukimuelewa Mourinho nn anakifanya kwenye kaz yake utamkubali tuu Mourinho nichocha mzuri nakira mtu ana mabayake kwaio nivitu vidogovidogo tuu vya kurekebishika anajua uyo
Elika
Namkubali sana jose mourinho
Kenani
Tunakwenda nawakati
Hamidu
kwa Jose Mourinho sitegemei Kama hataweza kufanya vizuri na timu za taifa.
Ngoja wait…!
Hope mwaikuka
Ipo siku asijal still namuan ni kocha nzur sana
Ester mmakasa
Asante meridianbet kwa taarifa.
Magdalena
Kashachuja uyo Hana jipya atulie tu
#meridianbet
Neema juma
Kocha mzuri sana huyo
Asia Abdy
saiv hana shuhuli
Theonestina
Asante kwa kutujuza
Aziza mushi
Mtu makini sana
Hidaya Mohammed
Kama ridhki yake ipo basi ataendelea na kazi yake
frank patrick
Team ya taifa bado huyo abaki na club tu kwanza
Samiah
Kocha km chocha atakiwa mbinu mmbadala
Agness
Nikocha mzuri asante meridani kwa taarifa
Povel
Thanks meridian bet kwa information
winfrida
mourinho namkubali sana uyu kocha
nasra
Namkubali sana
Tahiya
Bado ananafasi asikate tamaa
Emmy cleopa
Huyo kocha yupo vizur sana
Mwajuma
Asikate tamaa mungu anaweza akasaidia malengo yake yakatimia
Mariam mtandama
Duuuh
Mwanahamisi
Mtu Makini sana
Swai
Yuko vizuri na akiamua anafanya vizuri