Real Madrid wamekataa kumsaini nyota wa Brazili, Willian kwa uhamishe wa bure.
Mshambuliaji wa Chelsea, Willian atakuwa huru majira haya ya kiangazi wakati mkataba wake wa sasa utakapomalizika, anaweza kuondoka Stamford Bridge.
Real Madrid walionekana kumhitaji nyota huyo lakini miamba hiyo ya Hispania wapo tayari kumpa mkataba wa miaka mitatu.
Kocha Real Madrid, Zinedine Zidane anamkubali sana Willian lakini haoni kama anahitaji kuweka nguvu sana kumpata.

Wakala wa Willian, Kia Joorabchian amesema kipaumbele cha Willian ni kusalia Chelsea lakini ieleweke kama ataondoka Stamford Bridge atahamia klabu nyingine ya Premier League.
Tottenham na Arsenal wamehusishwa kumwania winga huyo lakini wameshindwa kukamilisha dili kwasababui ya kuyumba kiuchumi.
Joorabchian amesema: ”Willian alitaka kusiani mkataba wa miaka mitatu kupata mafanikio aliyoyataka kwa miaka mitatu na baada ya hapo aangalie wapi anaweza kwenda.
“Sera ya Chelsea kwa wachezaji zaidi ya miaka 30 atapewa mkataba wa miaka miwili tu kwahiyo tunapambana na hilo. Kwasasa Willian ana mkataba hadi mwisho wa msimu.
Willian amaitumika Chelsea kwa miaka saba tangu alipojiunga mwaka 2013, na ameshinda Ligi Kuu mara mbili, Kombe la FA na Kombe la Ligi.


Salma
Taharifa nzuri, kutokana ubora wake nadhani atachukuliwa sehem sahihi
David pere
Angekiwa kijanaa angewasaidia lakini yule mzee mpira wake ushamalizka tayari
Neema juma
Kote sawa atakavyoona yeye wapi pakwenda kwenye maslahi mazuri ataenda akitaka kubaki pia ni uamuzi wake
Hope mwaikuka
Panapomfaa aende tu
Zeiyana
Real Madrid bado wanamuitaji kiungo wao
Mwanaidi
Hawawezi kumuachia kirahisi rahisi ni jambo zuri walilolifanya Real Madrid
Antony Luseno
Lampard huyu jamaa bado anamhitaji asiruhusu aondoke
Rehema Dickson
atakavyoona yeye wapi pakwenda kwenye maslahi mazuri ataenda akitaka kubaki pia ni uamuzi wake
Shafii
Chelsea bado tunakazi nae ya kufanya
Rehema Dickson
kutokana ubora wake nadhani atachukuliwa sehem sahihi
Neema hassan
Willian fundii timu pinzan haziwez kumuacha kirahis..
Theckla
Bado tunakuhitaji
aisha
Baki tuu kaka william
Ester jackson
William mwamba sana namkubali vilivyo anajituma ipasavyo
felister
abaki tu
winfrida
Real Madrid walionekana kumhitaji nyota huyo lakini miamba hiyo ya Hispania wapo tayari kumpa mkataba wa miaka mitatu.bora asubiri dili hilo
Ester mmakasa
Baki tu mpambanaji ,bado tunahitaji uwepo wako.
Caroline
Mbna wana dharau Hawa…
Aziza mushi
Bado tunakuitaji mpambanaji ma shuhuri sana
Genia Sikaluzwe
Abaki tu kwa sababu huyo jamaa ni mpambanaji
amani
Sera ya Chelsea kwa wachezaji zaidi ya miaka 30 atapewa mkataba wa miaka miwili tu kwaiyo anaweza kwenda real madrid#meridianbettz
dorophina
Wasimruhusu haondoke bado mpira wake unaumuhimu
Lydia Emmanuel Magoti
Bado tunakuitaji mwamba
Magdalena
Abaki tu uko uko chelsea #meridianbet
Gabriel
Bora abaki Chelsea kwa mtazamo wng
Emmy cleopa
Abaki tu chelsea
Povel
Haondoke akatafute changamoto mpya
Mwajuma
Washamuna ni mzee miaka 32 sio kidogo kwenye soka
mathayo sonje
hili ni jembe ambalo chelsea watalikumbuka kama ataondoka, yuko vizuri, madrid wanalinga kwa sababu mkataba unaisha, wanataka dau dogooo, tumewashtukiaa!!!
Kenani
Atoke tu akapambane mbele kwa mbele
Ernest
Willian ni mchezaji hodari na bora, nadahni atapata timu ambayo atendeleza makali yake.
mwakalosi
huyu umri wake ni wakwenda juve sasa
Elika
Bado tunamuhitaji william.maana ni mchezaji hodari sana
Tahiya
Kutokana na umri kusogea nadhani asiweke masharti ya mkataba wa miaka 3 itamgharimu
Devotha
Ni mshambuliaji mzuri wachukue tu real madrid
Rehema
Huyo umri wake wa kubaki chelsea
Agness
Abaki asiondoke
Asha
Hatabak darajan awe mfalme tu
Frank Patrick
Zidane hataki mchezo
Theonestina
Chelsea kunamfaa zaid.abak tu