Nyota wa Arsenal Matteo Guendouzi hajafanya mazoezi na kikosi cha timu ya kwanza kwa zaidi ya wiki moja baada ya kupigwa marufuku na kocha wake Mikel Arteta. Mfaransa huyo amekuwa akifanya mazoezi binafsi pamoja na kocha wa viungo kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita kufuatia vitendo vyake vya utovu wa nidhamu kwenye mchezo waliopoteza 2-1 dhidi ya Brighton.

Guendouzi alibahatika kutopata adhabu kwenye mchezo huo lakini kocha wake Mikel Arteta ameonyeshwa kukasirishwa na tabia ya kiungo huyo na ameamua kumtupa nje ya kikosi chacke. Alipoulizwa juu ya suala hilo, Arteta amesisitiza mara kwa mara kuwa tabia ya mchezaji huyo haijabadilika na bado Guendouzi ana shida ya utovu wa nidhamu.
Kwa mujibu wa Jarida la Athlete, Guendouzi aliitwa katika mahojiano na Arteta pamoja na mkurugenzi wa ufundi wa klabu Edu baada ya tukio la kumkaba Maupay wa Brighton na wawili hao hawakuridhika na majibu yake wakati alipoulizwa maswali juu ya tukio hilo.
Mfaransa huyo ameambiwa atakuwa akifanya mazoezi peke yake na mbali na wenzake hadi akijirekebisha tabia yake. Arsenal ilimsaini kiungo huyo mkabaji kwa pauni milioni 5 kutoka katika klabu ya Lorient na anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji wenye nidhamu mbovu.

Kocha wa zamani wa Gunners, Unai Emery alikuwa akijua vyema matatizo ya utovu wa nidhamu wa Mfaransa huyo, ingawa alikuwa na imani angeweza kumbadilisha. Klabu sasa imepanga kukutana na wawakilishi wa Guendouzi katika siku zijazo kujadili mustakabali wake na inawezekana akaondoka klabuni hapo katika msimu huu wa joto.
Kwa sababu ya ukata wa kifedha wa Arsenal, klabu inaweza kupata pesa kwa mauzo ya kiungo huyo au kumtumia kama sehemu ya mabadilishano katika mkakati wake wa kumsaini kiungo wa Atletico Madrid Thomas Partey.


Rehema
Bonge la makala
Fatuma kasomo
Gud news
Hamidu
Dogo unAjua nenda katafute changamoto nyingine #meridianbettz
Caroline
Pole yake.aache kukiuka sheria
warda
Duuuu kesha jiaribia sasa#Meridianbettz
Mwanahamisi
Gud news
Adelta
Asante kwa makala nzuri
# meridianbet
felister
safi arteta hii itakua fundisho kwa wachezaji wengine apo klabuni
JULIANA
Nichangamoto tu za mpila,we nenda kajaribu kwengine
Neema juma
Mbona majanga kuwa moja wapo wa wenye nidhamu mbovu ila aombe samahani
Dorophina
Dogo anajua ndiomaana kiburi kingi lakini hakisaidii km ivyo baada ya kuwa uwanjani wamemuweka benchi
Magdalena
Sheria zimewekwa ili zifatwe sasa ujuaji wake katika mpira ndo afanye ivyo n makosa
David Pere
Yani hapo ulw usemi unaosema hakuna mxhezaji mkubwa kuliko timu Ndio inatimia Ndio maana wanammwaga
Angelina
Jeuri sio nzuri
Tatu
Utovu wa nidhamu sio nzuri unaweza ukajialibia
isha
Msameheni maisha mengine yaendelee kwa hakuna aliye kamilika
Genia Sikaluzwe
Ujeri sehemu ya kazi siyo mzuri
Shafii
Guendouz ni mchezaji mzuri ila kwenye mpira unapokua huna nidhamu hata Kama ni fundi kiasi gani ni rahisi kipaji chako kupotea.
Zuhura omary kindamba
Jeuri sio nzuri kwenye kazi
Samira
Ujuaji mwingi na jeuri sehemu pa kazi havina maana siku zote mwisho wake hua mbaya ndio kama kinachompata hapo
Evaluziga
Pole yake aache kukiuka sheria
Leonard
Bora aondoke
Salma
Sheria ifatwe
Emmy cleopa
Makara manzuri
Khadija
duh!! ujeuri sio mzr jamani kashajiaribia#meridianbettz
Theckla
Kiburi chake kimemponza
Tahiya
Nidhamu inahitajik
Saupha mohamed
Jeuli si uungwanaa
Flomena
Kwa sababu ya ukata wa kifedha wa Arsenal, klabu inaweza kupata pesa kwa mauzo ya kiungo huyo au kumtumia kama sehemu ya mabadilishano katika mkakati wake wa kumsaini kiungo wa Atletico Madrid Thomas Partey.# meridianbettz
Gabriel
Hv nice update 👍
Franky
Hutovu wa nidham co kitu kizuli so wamteme tu na co kumwaga pekeyake
Hope mwaikuka
Makala imeeleweka
Amiri Kayera
Nimaamuz ya harak wampe tena nafax
devotha
asante kwa makala
neema hassan
Kocha amefanya vizuri iwe fundisho kwa wengine..
Omary lukumbi
Acha tuu arteta amfundishe adabu maana anabidi awe na nidhamu
Aziza mushi
Pole yake
Ernest
Safi sana Arteta, hii nzuri sana atajifunza siku nnyingine
Sabrina
Maoni:Kweli Arteta mwalimu!
Zeiyana
Viwango vya wachezaji vinapotea kwa kukosa nidhamu.
Frank Patrick
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko team Arteta akiendelea hvyo atakuja kupata mafanikio sana kwenye kipindi chake cha ukufunzi
Povel
Utovu wa nidhamu co mzuri awe mfano kwa wengne