Mchanganuo wa Mechi ya Aston Villa Dhidi ya Manchester United

Villa hawakustahili kutoka mikono mitupu huko Anfield Jumapili iliyopita. Walijipanga vizuri kwenye safu ya ulinzi lakini wakashindwa kutengeneza nafasi za mabao.

Mchezo ungeweza kuisha 0-0 kirahisi, lakini game hiyo ikawa mfano halisi wa vilabu vikubwa vinavyo faidika zaidi na mabadiliko ya sheria ya sub 5, kutokana na kuwa na benchi bora na kikosi kipana kuweza kuchukua nafasi ya kushinda mchezo.

Liverpool iliweza kufanya mabadiliko makubwa katika kipindi cha pili cha mchezo huo na kupata matokeo. Ikumbukwe tangu Ligi irejee tena baada ya janga la corona, timu zinaruhusiwa kutumia sub tano, badala ya tatu.

Sidhani kama kulikuwa na haja ya kufanya mabadiliko ya sheria hii kwenye mchezo, na kile kilichofanyika kimezipa faida timu zote za juu kwani zina vikosi vipana, hivyo zinapata nafasi ya ziada ya kuongeza ubora kwenye mechi.

 

Naweza kusema hii ni mojawapo ya sababu kubwa kwa nini timu nne za chini EPL zimepoteza sana michezo yake tangu kurejea kwa Ligi, na hii itakuwa shida nyingine kwa Aston Villa kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya United.

Man United wana kikosi kipana, na ikiwa mambo hayataenda sawa kwao wanaweza kuingiza nyota wao mwingine wakabadilisha matokeo. Vijana wa Ole Gunnar Solskjaer ndio timu iko fomu bora kabisa katika ligi kwa sasa, hawajapoteza katika michezo 9 iliyopita ya ligi, wakishinda michezo sita na kupata sare 3.

45 Komentara

    asante kwa mchanganuo huo ila pongezi kwa man united

    Jibu

    Maoni:Asante kwe taarifa

    Jibu

    Don’t miss SAMA goaL vs RASHfOrd

    Jibu

    Man u wapo moto sana ila aston villla wanatakiwa kushinda mechi yao dhidi ya man u ili kujikwamua kutoka chini kabisa ya kushuka daraja pia na man u wanakipengelee kizito cha kupigania big 4 sasa hapo ndipo baraa zito

    Jibu

    Kwa namna nyingine unaweza kuiita Vita ya uzoefu dhidi ya ufundi. Hii ni kwa sababu makocha wa timu hizi mbili kuwa na falsafa zinazotofautiana. Van gaal yeye anaamini uzoefu wa wachezaji wake katika kuhimili presha za timu ndogo ndio utakaowapa ushindi leo katika dimba la villa park, wakati Tim Sherwood yeye anaamini njia zitakazowapa ushindi leo ni kitumia vizuri mbinu zake za kiufundi ili kuwamaliza kabisa wapinzani wao.
    Hali ya vikosi kwa upande wa timu zote ni nzuri kwani Manchester united itaingia dimbani pasipokuwa na majeruhi yeyote isipokuwa kuna baadhi ya wachezaji tu wamepumzishwa kutokana na sababu mbalimbali.
    Baadhi ya watu waliopumzishwa ni pamoja na golikipa namba moja David de gea, na beki kisiki Marcos Rojo. Kwa upande wa Aston villa pia hawana majeruhi ya kutisha ila tu kasi yao ya uchezaji inaweza athiriwa kwa kuwakosa wachezaji wake muhimu waliotimkia timu pinzani kama vile Benteke na Delph.
    Wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hizi wana mengi ya kuonesha kwa sababu ligi bado mbichi.. mshambuliaji Ayew wa aston villa alianza vizur kwa kupachika bao hvyo wengi wanasubiria kuona kama kasi yao itaendelea ama la. Kwa upande wa manchester united bado mchezaji wao anaetegemewa kwa makubwa hajaanza kuonesha cheche zake.
    Hii ni labda sababu van gaal anamchezesha namba tofaut na aliyozoea, endapo akiwekwa huru kwenye namba aliyobobea basi tutarajie makubwa sana toka kwa Memphis.. Morgan na Darmian waliamza vizuri mnoooo na mengi hakika yatarajiwe toka kwao.
    Utabiri wangu kwa siku ya leo ni kuwa na mechi ngumu sana ambayo ni lazima kwa timu zote kufungana. Matokeo ya mwisho yatakuwa ni Aston villa 1-2 Manchester united

    Jibu

    Ningependa kuona Samata akibaki Ligi kuu ya EPL lakini wanahitaji maajabu kuendelea kuwepo EPL#meridianbettz

    Jibu

    mambo ni moto na meridianbet

    Jibu

    Hii ni labda sababu van gaal anamchezesha namba tofaut na aliyozoea, endapo akiwekwa huru kwenye namba aliyobobea basi tutarajie makubwa sana toka kwa Memphis.. Morgan na Darmian waliamza vizuri mnoooo na mengi hakika yatarajiwe toka kwao.
    Utabiri wangu kwa siku ya leo ni kuwa na mechi ngumu sana ambayo ni lazima kwa timu zote kufungana. Matokeo ya mwisho yatakuwa ni Aston villa 1-2 Manchester united

    Jibu

    Dante meridianbettz kwa update za michezo

    Jibu

    Hapa namwombea Man U ushindi tu#Meridianbettz

    Jibu

    Ahahaa…so nice mpira dk90 banaa

    Jibu

    Astovilla anauwez ten

    Jibu

    Mchezo mkali sana ila daah astoni Villa sijui Kama atamfunga man u… Ila anatakiwa akaze ili hijinusuru kushuka daraja

    Jibu

    Asanteni kwa taalifa Meridianbet

    Jibu

    Man U ushindi wake

    Jibu

    Man United leo ushindi lazima mbio za kuwania top four tukiwa tunakimbizana na Chelsea ambae bado anapambania kubaki top four epl imepamba moto sana kipindi hiki cha kwisha kwa ligi kuu kuwania tiket ya kushiriki uefa champions league msimu ujao vijana wa ole gunnar wana sumu kali ya kumuangamiza kila anae kuja mbele yao Aston villa wanajitahid kupambana ili kujinasua kutoka kwwnye hatar ya kushuka daraja mungu atawasaidia lakin si kwa mechi ya leo maana point 2 tofaut kuanzia nafasi ya tatu mpaka ya sita mbili mbili tinu zilivyo pitana hii vita ya kufa mtu

    Jibu

    Mtanange hatari villa wajipange

    Jibu

    Aston villa wanahitaji nguvu ya ziada ili kuti walilokalia lisikatike

    Jibu

    Ushindi kwa timu yangu man u

    Jibu

    Leo kazi ipo

    Jibu

    Aston Villa lazima washuke daraja kwa kuwa Man U wanatafuta nafasi ya kushikiki UEFA kwahiyo hawatamuacha lazima wampige tu

    Jibu

    Aston villa inabidi wafanye kazi ya ziada ili kujikwamua wasiweze kushuka dataja na tuendelee kumuona kijana wetu Samatta

    Jibu

    Ushindi kwa man u

    Jibu

    Sub tano zinawafaidisha timu kubwa

    Jibu

    Man u ushindi lazima

    Jibu

    Man u ushindi lazima

    Jibu

    Man u nilazima ashinde magoli mengi

    Jibu

    Man u namuombea ushindi ili achukue nafasi ya nne

    Jibu

    Aston villa inawaweza man kweli

    Jibu

    Apo mm nataka Man U ashinde tuu Samata utanisamehe kwakweli mtanange huo

    Jibu

    Man u ushind lazima#meridianbettz

    Jibu

    Mechi hii nikama baba alicheza na mtoto wake mpira ikiwa mtoto yupo mdogo sana daaah Aston villa wajipange vizuri kwa Mara nyingine

    Jibu

    Hali ya vikosi kwa upande wa timu zote ni nzuri kwani man chester itaingia dimbani pasipo kua na majeruhi yoyote isipokua kuna baadhi ya wachezaji wamepunzishwa kutokana na sababu mbali mbali

    Jibu

    uzalendo kwanza #Lydia

    Jibu

    Nawaonea aston villa huruma watafungwa

    Jibu

    Mtanange mkali sana huu

    Jibu

    Asante meridianbet #kwa taarifa

    Jibu

    Duuh Asto villa inaweza kweli jamani

    Jibu

    Dahh Aston villa inabidi mkaze buti sana

    Jibu

    Safari ya Aston villa kushiriki EPL msimu kesho ndo inaishia hapa poleni Sana.

    Jibu

    Duuh nawaonea uruma tu Aston villa apo #Meridianbettz

    Jibu

    Aston Villa wamekubwa na kirusi cha Corona, timu imekuwa mbovu sana sio tena ya ushindani kama hapo awali.

    Jibu

    Mmmh Aston villa itaweza kwelii

    Jibu

    Imeeleweka

    Jibu

    Naweza kusema hii ni mojawapo ya sababu kubwa kwa nini timu nne za chini EPL zimepoteza sana michezo yake tangu kurejea kwa Ligi, na hii itakuwa shida nyingine kwa Aston Villa kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya United.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.