Floyd Mayweather ametangaza kustaafu mara tatu!
Ni bondia ambaye amejijengea umaarufu mkubwa kwa uwezo wake ulingoni akifanikiwa kushinda mapambano yake yote 50 aliyopambana. Pia amejizolea umaarufu zaidi kwa utajiri alionao, huku akitamba kwa jina la “Money” na timu yake ikiitwa “Money Team” au “Team Money”.
Licha ya uwezo wake Ulingoni, bingwa huyu ametangaza kustaafu mara tatu. Kwa mara ya kwanza Mayweather alitangaza kustaafu mwaka 2007 baada ya kumtandika KO Ricky Hatton kwenye raundi ya 10.
Miaka miwili baada ya kustaafu Mayweather aliamua kutinga tena ulingoni kupambana na Juan Manuel Marquez, ilikuwa 2009. Katika kurejea kwake alipata ushindi katika mapambano 10, yakiongezeka katika mapambano 39 aliyoshinda kabla ya kutangaza kustaafu.
Katika mapambano 10 ya kurejea kwake alishinda jumla ya dola milioni 600. Alitangaza kustaafu kwa mara ya pili mwaka 2015 baada ya kuchapana na Andre Berto na kukamilisha rekodi ya mapambano 49 bila kupigwa. Hapa alikuwa na umri wa miaka 38.
Kwa mara ya tatu, Mayweather alitangaza kustaafu mwaka 2017 baada ya kurejea na kumpiga Conor McGregor katika raundi ya 10. Pambano hili lilimuacha na kitita cha dola milioni 275. Hapa alikamilisha mapambano 50 katika ndondi za kulipwa bila kupoteza pambano.
Ametangaza Kustaafu lakini yupo Mchezoni!
Kwa sasa anamiliki klabu ya bosing ya “Mayweather Boxing Club”. Na anafundisha na kufanya mazoezi ili kuendelea kuwepo kwenye fomu nzuri. Licha ya kutangaza kustaafu, mbado yupo tayari kuruka ulingoni kila anapopata ofa ya hela kubwa.
Wengi wanaona kuwa bingwa huyu asipoamua kustaafu mazima akiwa na rekodi yake nzuri aliyonayo, basi atastaafu kwa lazima kwa aimu ya kupoteza pambano.
Wewe una mtazamo gani? Nitafurahi kusoma maoni yako hapa chini.
Una nafasi ya kubashiri michezo mingi kadri uwezavyo hapa na Meridianbet
Caroline
Floyd Mayweather bonge la bondia yn
Ernest
Floyd Mayweather- Team money napenda kumuita mzee wa kupiga pesa tuu yeye ndo ufahari wake
devotha
bado anauwezo sana hakuna haja ya kutangaza kustaafu kila mara
Lydia Emmanuel Magoti
Floyd Mayweather bonge labondia mtu wakupiga pesa namkubali achoki akili nyingi huyo jamahaa
Sabrina
Maoni:Floyd Mayweather hana masihala akiwa ulingoni jamaa mbabe wa ulingo
Dorophina
Mayweather umri umeenda lkn bado yupo vizuri mzee wa kutengeneza bingo uwanjani ngumi yake si ya kitoto
Magdalena
Mayweather yupo vizuri Sana katika ngumi namkubali
Genia Sikaluzwe
Floyd Mayweather ni bondia anaejali kazi yake ya gumi
Sadick
Ningependa aendelee kuonyesha uwezo wake ulingoni#meridianbettz
Gabriel
Floyd Mayweather n bonge la bondia huyu namkubal sana kwa style yake ya uchezaji ngumi ni bondia ambaye mwepesi sana kuwepa Mayweather ameingia katika rekodi ya mabondia wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi kwa mwaka, pambano lake la mwisho la mwaka 2015, kabla ya kustaafu, alimpiga bondia kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao mwenye urefu wa futi tano na nchi 5, na uzito kilo 66, baada ya kuibuka mshindi katika pambano hilo mashabiki walimpachika jina la The Best Ever au T.B.E.
Bondia huyu ambaye pia ni mjasiriamali ana miliki akaunti moja ya benki yenye zaidi ya dola milioni 123 ndani yake.
Mayweather ni kiongozi wa kundi liitwalo The Money Team (T.M.T), na upande wa pili wa maisha ya kimapenzi, bado hajaoa hadi sasa ila ni baba wa watoto wanne kwa wanawake tofauti, mpenzi wake wa awali Jossie Harris amezaa naye watoto wawili wa kiume Koraun na Zion, na mmoja wa kike anayeitwa Jirah.
Mtoto wake wa mwisho anaitwa Iyyana, amezaa na mpenzi wake mwingine, Mellisia Brim. Alishawahi kutumikia kifungo jela huko Las Vegas kwa kosa la unyanyasaji na vurugu ila namtambua Kama bondia tajir mwenye mafanikio sana π
Povel tz
Gud news
Hamidu
Mpiga pesa huyoo Mayweather #meridianbettz
Njiku
Gud news
lombo
duh
Rehema Dickson
bonge labondia mtu wakupiga pesa namkubali achoki akili nyingi huyo jamahaa
Furahav
Namkubali sana.
warda
Namkubali sana Mayweather#Meridianbettz
Franky
Bondia Atari sana uyuu…#meridianbet
Amiri Kayera
Vizur bad anapg pesa
Edgar
nakubali
Zuhura omary kindamba
Ningependa mayweather aendelee kuwa na kipaji zaidi
Omary lukumbi
Mzee wa TMT “the money team” flody mayweather ni bingwa wa ndondi dunian ila nakumbuka pambano lilo shika vichwa vya watu lile alopigana na man pacquao lilisisimua watu maana lilikua na mvuto kuona mabibgwa wakitwangana ni mtu mwenye utajiri mkubwa na umri mdogo amekua maarufu sana kwa uwezo wake anao onesha ulingoni team yake
neema hassan
Mayweather bondia hatari
Theckla
Ingefikia hatua awaachae wanafunzi wake
Theonestina
Namkubar Sana uyo bondia
Salma
Wanapenda sana kuonekana wao waache vipaji vipya navyo vijulikane
David Pere
Huyu jamaa no chizi wa pesa japo anasema amestafu lakini Kama kutatoke mtu mwenye mpunga anatudi na kuzichapa ili apate pesaaa
Revina
Ni bondia ambae anajiamini na ana jua anachofanya ,ila ana sifa sana ,ila hana mpinzani
Aziza mushi
Yupo vizuri Sana.
Leonard
Anasubiri astaafu kwa kipigo
Fatuma kasomo
Yupo vizuri aendelee tu kuonyesha uwezo wake ulingoni
Mwanahamisi
Yuko vizuri sana
Tatu
Good news
Khadija
Namkubali sana mayweather mpiganaji anayejikubali bondia asiyekubali kupiga#meridianbettz
Hidaya
Kazi na umri
Ester jackson
Floyd Mayweather n bonge la bondia huyu namkubal sana kwa style yake ya uchezaji ngumi ni bondia ambaye mwepesi sana kuwepa Mayweather ameingia katika rekodi ya mabondia wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi kwa mwaka. Pia alionyesha kuguswa sana na tukio la ubaguzi wa rangi lililotokea nchini marekani kwa kijana Floyd mpaka kupoteza maisha lakini aliweza kuchangia pesa za mazishi yake huo ni uungwana ambao unaonyesha UPENDO kwa watu .#meridianbettz
Zeiyana
Siku ambayo hatapigana ulingoni na kushindwa kwa raund
Zeiyana
Siku akipigana ulingoni akapigwa kwa raond moja tu ndio hata staafu kucheza
felister
ni bondia aliyejijengea umaharufu mkubwa akiwepo ulingoni
Rehema
Aiseee!
Shafii
Huyo jamaa anaseti pambano rahisi ajizolee sifa na pesa Hana lolote.
Samiah
Safi
Saupha mohamed
Jamaa namkubalii sanaa
Hope mwaikuka
Atulie na yy pesa si ipo
Flomena
Kazi na umri aachie ngazi tu
Issa
Moneyman ni noma sana rekodi isiyofutika na hela ndefu