Wachezaji Mastaa Waliopitia Msoto.

Luis Suarez. 

Staa wa soka wa timu ya taifa ya Uruguay ambaye kwa sasa anaichezea FC Barcelona ya Hispania, Ni moja ya wachezaji waliopitia msoto, akiwa na umri wa miaka 12 Suarez alikuwa akicheza mpira pekupeku kutokana na familia yake kushindwa kumudu kumnunulia viatu.

Suarez amezaliwa katika familia ya watoto saba yeye akiwa wanne na akiwa na umri wa miaka 9 baba na mama yake walitengana, Suarez wakiwa Montevideo aliendeleza kipaji chake kwa kucheza mtaani lakini pia alikuwa akifanya kazi za kufagia mtaani.

Wachezaji Mastaa Waliopitia Msoto.

Luka Modric. 

Moja kati ya viungo bora wa timu ya taifa ya Croatia na Klabu ya Real Madrid ya Hispania, lakini akiwa na miaka 6 mwaka 1991 vita vya Croatia ambavyo vilimpelekea baba yake kujiungana na jeshi, vilimfanya yeye na familia yake kwenda kuishi Kolovare katika kambi ya wakimbizi kwa miaka saba.

Wachezaji Mastaa Waliopitia Msoto. Wachezaji Mastaa Waliopitia Msoto.

Carlos Tevez.

Amewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya kama West Ham,Man city na Man United na sasa yupo kwao Argentina anaichezea Bocca Junior.

Tevez amekulia Fuerte Apache nchini Argentina moja kati ya sehemu hatari zaidi duniani na wanaishi watu masikini na kuna matukio mengi ya kiharifu na uuzwaji wa dawa za kulevya.

Kuharibika kwa meno yake kunatokana na matukio ya ugomvi aliyokuwa anapitia katika mtaa aliokulia.

Wachezaji Mastaa Waliopitia Msoto.

Cristian Ronaldo.

Moja kati ya wanamichezo matajiri katika hii dunia kwa sasa. Mara yake ya kwanza kupanda ndege ilikuwa ni wakati anakwenda kusaini Man United.

Kabla ya hapo Ronaldo amekulia katika familia ya kimasikini Ureno na ilifika wakati akawa analala chumba kimoja na dada zake kutokana na ugumu wa maisha licha ya kuwa umri ulikuwa unataka awe na chumba chake.

Dani Alves.

Amecheza FC Barcelona, Juventus, PSG na sasa Sao Paulo ya Brazil, Alves wakati akiwa mdogo alikuwa akilazimika kuamka saa 10 alfajiri ili kwenda na baba yake kumsaidia katika shughuli zake za kila siku.

Alikuwa akilala katika kitanda kibaya, pamoja na ugumu wa maisha hayo aliyoyapitia Alves amewahi kukiri kuwa alikuwa ameridhika nayo.

Zlatan Ibrahimovic.

Ambaye ameichezea Man United,LA Galaxy ya Marekani na sasa Ac Milani ya Italy alizaliwa wilaya ya Rosengard katika mji wa Malmo nchini Sweden.

Zlatan amekuwa akiwa na sifa mbaya na ametokea katika familia ya kimasikini, baiskeli aliyokuwa anaitumia kwenda nayo mazoezini ilikuwa ya wizi.

Wachezaji Mastaa Waliopitia Msoto.

Neymar JR.

Ambaye kwa sasa anatazamiwa kuja kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa miaka ya baadae, amelelewa  katika nyumba ya babu yake ambapo alikuwa analelewa katika chumba duni sana na alikuwa akishea chumba hicho yeye, wazazi wake na dada yake.

Sarakasi za Usajili wa Neymar, Mnamuelewa Kweli?

 

Alex Sanchez.

Kwa kiasi kikubwa maisha yake ya utotoni amelelewa bila uwepo wa baba yake na alikuwa akifanya kazi za kuosha magari ili aweze kuisaidia familia yake nchini Chile.

Sanchez anamini kama sio mpira basi asingekuwa chochote katika hii dunia.

Inter Milan wanamtaka Sanchez Mazima.

Frank Riberry.

Amekulia ghetto Kaskazini mwa nchi ya Ufaransa na aliepuka kuishi maisha ya bila kuwa na kazi kwa kuanza kufuata ndoto zake za kucheza mpira kitu ambacho kimemkomboa katika maisha yake na kufanya dunia nzima kumjua kwa uwezo wake.


                                      Cheza Kasino za Mitandaoni   

                                                       Bofya hapa

Break da Bank Again ni Sloti Bomba ya Kasino ya Mtandaoni   

48 Komentara

    Duuh

    Jibu

    Mafanikio bwana yanakuja kwa tabu sana, Asilimia kubwa msoto kwanzaaa baadae ndo mteremko

    Jibu

    Duuh mengine nilikuwa sijui aisee kama zlatan mpka baiskel ya wizi leo bonge la staa

    Jibu

    kweli ili ufanikiwe lazima upite kwenye msoto

    Jibu

    Duh kwl mafanikio ni kupamban kwl hawani kioo kwl kwetu hakun kitu cha slope kwny kutafut mafanikio thnks meridian bet kwa update za burudan na michezo

    Jibu

    Daah mungu ni mwema akunaanaejua kesho yeke…makala mzuri

    Jibu

    Ni kweli ili ufanikiwa lazima upitiy changamoto

    Jibu

    Kazi ya ustaa ni ngumu maana asilimia ya mastaa wengi wanapataga shida sana

    Jibu

    Msoto uliowakuza hapa walipo hawakukata tamaa

    Jibu

    Mpaka kuja kumfikia mafanikio lazima upitie msoto

    Jibu

    Duu nikweli ili ufanyikiwe lazima upitie changamoto zakila dizain

    Jibu

    Kweli wamepitia hali ngumu mpaka kufikia mahali pazuri

    Jibu

    Mmh

    Jibu

    Asante kwa kutuletea makala nzuri ya kusisimua#meridianbettz

    Jibu

    Mafanikio huja na msoto so safi sana kwao

    Jibu

    Maisha ni safari ndefu sana.

    Jibu

    Hakuna kitu kinakuja Kwa urahisi

    Jibu

    Maoni:Duuh wameishi maisha magumuu ila walipambana kwaajili ya kesho yao

    Jibu

    Wamepigia ndoto mkali lakini Sasa hivi nibmadoni kinoma na wanaheshimika kuliko hata viongozi wa nchi zao

    Jibu

    Duuh ili ufanikiwe upitie magumu

    Jibu

    Nice update 👍

    Jibu

    Bill Gate anasema ukizaliwa masikini sio kosa lako lakini ukufa masikini ni kosa lako. wenzetu walijua karama Mungu ameweka ndani yao na wakaitumia kufanikiwa. Tatizo la wengi kushindwa ni kuridhika na hali mbaya wanayokutana nao maishani#meridianbettz

    Jibu

    no body knows about tomorrow

    Jibu

    Duh kupitia kipindi kigumu ndio kinaleta mafanikio katika maisha hongereni Sana wachezaji

    Jibu

    Duuuu!!!Kweli haya Maisha usikate Tamaa!#Meridianbettz

    Jibu

    Duh watu wanaptia changamot

    Jibu

    Duuh watu wanatoka mabali sana ila kwangu nimejifunza kitu kupitia mastaa hao…. Asante meridian¥

    Jibu

    Maisha safari ndefu

    Jibu

    Duuh ina sikitisha ila pia inatutia moyo pia kwa wale ambao bado hatujafanikiwa maana uvumilivu wao ndio umefanya wapate kile ambacho walicho kiangaikia kwa muda mrefu utajir hauji kirahisi kama kutia chakula mdomoni au kusukumizia jiwe shimon

    Jibu

    Hongera yao kwa uvumilivu

    Jibu

    Chochote unachokitaka utakiwi kukata tamaa walivumilia vya kutosa na sasa wanaona matunda yake

    Jibu

    Maisha watu wanatoka mbali kweli

    Jibu

    Duniani haitakiwa kukata tamaa

    Jibu

    Mafanikio hayawezi kuja kwa miujiza lazima upambane ,ndo maana wanasema fanya kazi kama mtumwa ili uje uishi kama mfalme

    Jibu

    Wamepitia msoto mkari Sana lakini Sasa hivi ni madoni minimal

    Jibu

    Asilimia kubwa msoto kwanzaaa baadae ndo mteremkoTatizo la wengi kushindwa ni kuridhika na hali mbaya wanayokutana nao maishani#meridianbettz

    Jibu

    Hongera kwa uvumilivu

    Jibu

    Mafanikio ayaji kwa njia rahisi

    Jibu

    Ni historian ya kusisimua ambayo ina mafunzo ndani yake kuwa masikini katika familia sio mwisho wa maisha ni hakili na juhudi katika nia uliyo iweka asante meridian kwa nakala

    Jibu

    Nimekubali kweli haya maisha usikate tamaa#meridianbettz

    Jibu

    Ronaldo amepitia maisha magumu sana kuna badhi ya maisha uwezi kuyasahau katika histor yako kwa kweli

    Jibu

    mafanikio bwana yanakuja kwa tabu sana

    Jibu

    Duuu!

    Jibu

    Siku zote wanao pambana ndio wanaofanikiwa.

    Jibu

    Asante kwataharifa,maana nimejua nisiyoyajua

    Jibu

    Nlkua sijui hii axante kwa kunijuza

    Jibu

    Maoni:mtafutaji achoki

    Jibu

    Mafanikio bhana ni Kama dhahabu ichomwe kwenye Moto ndio ing’ae

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.