Tarehe 22 mwezi Novemba 1986 ndio siku ambayo Mike Iron Tyson alikuwa na umri wa miaka 20 ambapo alishinda ubingwa wa ndondi katika uzani mzito zaidi duniani akiwa na umri wa miaka 20 na hivyobasi kutangazwa kuwa bondia mchanga zaidi wa uzani mzito kuwahi kushinda taji hilo baada ya kumshinda Trevor Berbick.

, Mike Tyson Aamsha Hisia za Mashabiki wa Ndondi, Meridianbet

Zaidi ya miaka 33 baadaye, bondia huyo wa zamani alietia fora bado anaweza kujivunia kuwa mtu hatari zaidi duniani.

Tyson mwenye umri wa miaka 53 anathibitisha kwamba tabaka linaweza kudumu baada ya kuchapisha kanda yake ya video akifanya mazoezi ya kupiga begi na kufanya mazoezi ya ndondi.

Bondia huyo alisambaza video fupi ya sekunde tano ikimuonesha akifanya mazoezi  akiwa na kasi,nguvu na ukali iliyopelekea wapenzi wa masumbwi duniani kote kutoa maoni yao kuhusu ubora wa Mike Tyson.

Watu maarufu katika ndondi, na burudani walikuwa wa kwanza kutoa maoni yao.

Mwanamieleka aliyebadilika na kuwa muigizaji wa filamu kwa Jina Dwayne ama ‘The Rock’ Johnson alisema: Narudi katika mazoezi.

, Mike Tyson Aamsha Hisia za Mashabiki wa Ndondi, Meridianbet          Mike Iron Tyson

Nyota wa mchezo wa UFC Khabib Nurmagomedov alisema: Siwezi kuamini. hiki ni kiwango chengine.

Nyota wa filamu Will Smith alimuita ”shujaa wangu” huku Mfalme wa Podcast Joe Rogan alitumia lugha tofauti kuonyesha furaha yake.

Watu wengi walijadili kuhusu video fupi hiyo iliyo sambazwa na mkali huyo wa ngumi duniani.

David Haye  alisema “Bado ni mtu mbaya sana katika hii sayari” pia rais wa WBC  Mauricio Sulaiman alisema “Tyson ni wa maajabu!”

46 MAONI

  1. Hatar Sana bondia Mike Tyson amejitengenezea historian Safi Sana dunian kipind Cha yy alipokuwa ulingon

  2. Ni habar njema sana 👍 kumhusu kwan mashabiki tunamtambua Mike Tyson Kama bingwa wa dunia maana alianza ngumi akiwa na umri mdogo sana nakumbuka akiwa na umri wa miaka 15 alishawai kuchukua medal ya olimpic na pia mwaka mwingne akiwa na umri wa miaka 16 akachukua nyingine hivyo kipaji chake kilianza akiwa na umri mdogo sana
    Mei 23 2017 mike Tyson alishawai kusema kupitia jukwaa la salt conference chin ya CNN namnukuu Kama shabiki yake alisema sikudhan Kama angefika miaka 30 maana alijua atakuwa amekufa kutokana na mambo ambayo alivyokuwa anayafanya Kama uvutaji wa bangi kupita kiasi ,unywaji wa pombe kal sana na matumiz ya madawa ya kulevya na mawaka ulimwingne alishawai kuzuiliwa ital asiingie kwenye tamasha na polisi ila baadae akaacha vyote na kuwa mtu wa kawaida kwa upande wangu namkubal sana 👍 huyu jamaa natumain ipo siku tutampata mrithi wake

  3. Mikel tyson ni mtu hatar sana kwenye masumbwi umalizi raund zote bila kwenda chini na kumnyanyua kua bingwa tyson kwenye pambano lake unaweza kata tiket unaingia ndan tuu unaambiwa pambano limeshaisha mtu yuko chini hii ni storia ya kipekee

  4. Kwa sisi ambao hatujawahi kumshuhhdi akizichapa lazima tutakuwa na hisia kubwa Sana za kutaka kukuona akipogana tena

  5. Mike Tyson ndio alikua bondia hanayependwa kwa kila kijana ambaye aliyekua hanijifunza michezo ya ngumi alikua kivutio kwa vijana wengi na kutaka kua kama alivyo yeye

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa