Kiungo wa timu ya West Ham, Declan Rice ameombwa apotezee dili la kwenda Chelsea na nyota wa mchezo wa mieleka Triple H.
Triple H ambaye ni bingwa mara 14 wa WWE, ni shabiki mkubwa wa West Ham na kamwe asingependelea kuona Rice anaondoka klabuni hapo licha ya tetesi za nyota huyo kuhamia Chelsea kupamba moto siku za karibuni.
Nyota huyo wa mchezo wa mieleka amemtumia Rice ujumbe wa wazi katika mtandao wa kijamii juu ya umuhimu wa yeye (Rice) kuendelea kuwatumikia West Ham kuliko kuhamia timu nyingine.
Rice, mwenye miaka 21, amekua akihusishwa na tetesi za kurejea katika klabu yake ya utotoni, Chelsea iliyomuuza kwa West Ham miaka 7 iliyopita akiwa na miaka 14 tu!

“Msimu mpya unaanza, ninao ujumbe kwa Declan Rice”, alisema Triple H katika sehemu ya video aliyoichapisha katika mtandao wa Twitter.
“Declan (Rice) naelewa kuwa unayo maamuzi makubwa mbele yako, najua pia kuwa sina mamlaka yoyote kukuamulia nini cha kufanya, lakini ningependa kukupa ushauri juu ya hilo. Kukuonesha kwamba kwenye maisha kuna vitu vya muhimu zaidi.
“Zipo fursa za kuwa shujaa, shujaa kwa mashabiki waliokuunga mkono kwa miaka nenda rudi! Kuwa shujaa kwa watu walkokuona ukikua katika mfumo, na kufanikiwa ndani ya mfumo huo.
“Baki na watu waliokufanya kuwa hivyo ulivyo leo, baki na West Ham na uendelee kuwa shujaa wetu, Kuwa bingwa, uwe vyovyote vile unavyoweza kuwa na sisi.”
Ikumbukwe kuwa, Rice ana mkataba wa kuendelea kubaki na West Ham mpaka 2024, na mkataba wake unamruhusu kufanya maamuzi ya kukubali au kukataa usajili wa timu yoyote itakayomhitaji.
Rice amekua na kiwango bora msimu ulioisha (2019/20) kiasi cha kumshawishi kocha wake, David Moyes amchezeshe katika mechi 39.
Nyota huyo amecheza mechi zote za Ligi Kuu za West Ham kwa msimu uliopita huku akifunga magoli matatu na kutoa pasi saba za magoli, huku akivaa kitambaa cha unahodha mara nne.
SHINDA NA HI LO
Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.


Rehema
Duuh bonge la makala
Johnmary joel
Maamuzi yake Declan rice kuondoka au kubaki#meridianbett
Dorophina
Sio mbaya kama Ni Chelsea ndio timu iliyomrea sidhani kama Kuna ubaya yeye kurudi nyumbani alipokulia kuendelea na soka
magdalena
yeye ndo mwenye maamuzi ya kujua wappi panamfaa zaidi
Mwajumah
Ayo ni maamuzi yake binafsi kuamua kuondoka au kubaki chelsea#Meridianbettz
aisha
Ni maoni km shabiki lakin kila mchezaj anataman kufikia mafanikio yakuchez big team
Shani
Ni juu yake sasa mengine ni ushauri athima iko kwake!!
Adelta
Yeye ndiye mwenye maamuzi
@meridianbettz
Ernest
Binafsi naona Rice amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Westham lakini katika kucheza soka lazima uangalie na faida hapo mbeleni kama kutatokea na deal zuri kwa Rice hana budi kulifukuzia
Caroline
Declan baki West Ham wamekufanya ivo ulivo.
Nasra
Uamuzi mzur upo kwake
Mwanahamisi
Gud news
felister
maamuzi anayo yeye mwenyewe Triple H hauna mamlaka yeyote ya kumuamulu nini afanye na nini asifanye
Lydia Emmanuel Magoti
Yeye ndio mwenye mahamuzi afanye mamuzi yeye Kama yeye
Furahav
Duuh
Khadija
Maamuzi anayo mwenyewe ss wengine wasikilizaji tu#meridianbettz
Hidaya
Wamuache mwenyewe achague anapotaka kwenda
Tatu
Maamuzi anayo mwenyewe kubaki au aende
Povel
Nice information
Saupha mohamed
Yeye ndo mwenye maamuzi
Sauda
Kuondoka au kubaki ni uamizi wake mwenyewe
Frank P
Big asset kwa westham
Fatuma kasomo
Maamuzi anayo yeye
Agness
Habari njema
Amiri Kayera
Maamuz yake Ila ni ndoto za wachezaj wengi kuchez team kubw
Neema
Maamuzi anayo yeye
Theonestina
Duuuh
Rose kapinga
Mmmmh!!! Maneno hayoo!!! Ila maamuzi anayo mwenyw
Genia Sikaluzwe
Maamzi Anayo mwenyewe
Sabrina
Triple H nae fitina kweli atamlipayeye sasa amuache mwenzie aangalie masirahi yake aache habari zake za ushabiki
Shafii
Siku zote maamuzi ya mtu hayapangiwi.
Hope mwaikuka
🙌
Sadick
Declan Rice alikuuzwa kwenye academy ya Chelsea ilikuwa ni sawa na kurudi nyumbani pengine maombi ya Triple H yanaonekana kutimia#meridianbettz
Gabriel
Ayo ni maamuzi yake binafsi kuamua kuondoka au kubaki
warda
Maamuzi ni yake mwenyewe