Beki wa Chelsea – Thiago Silva, anasema kwake ‘umri ni namba tu’. Sio sababu ya kushindwa kuendana na kasi za EPL.
[Thiago] Silva amesajiliwa kama mchezaji huru akitokea PSG japokuwa anaumri wa miaka 36 kwa sasa. Mpaka sasa hajaitumikia Chelsea, japokuwa kuna uwezekano akacheza dhidi ya Barnsley kwenye Mashindano ya Carabao.
“Sinashaka kabisa kwasababu ninajua ninapotaka kufika. Nina imani kubwa na timu hii ya vijana.
“Ninajisikia vizuri, umri ni namba tu kwenye taarifa zako. Mimi ninajisikia bado mdogo sana, nilijiandaa kwa muda mrefu.
“Watu wanaonifahamu, wanajua ninawekaga 200% kwenye kazi yangu. Hii ni fursa kubwa ya Chelsea na Lampard kuniamini na sitaki kuwaangusha.
“Sijawahi kujiona kwenye EPL kwa sababu nilidhani ni mfumo mgumu wa kucheza soka. Sikua natamani kucheza EPL kwasababu navutiwa na mpira wa pasi ndefu na mashuti.
“Sikuwa ninatamani ila baada ya muda mambo yalibadilika na kuanza kuvutiwa baada ya kuona ubora wa kiufundi. Timu nyingi zinamiliki mipira, wanashambulia kwa kutumia walizi wa pembeni na kila timu ina namna yake ya uchezaji.
“Ninajua namna ya kucheza hivyo lakini ninapenda kucheza na mpira. Ninaujua ubora wangu, taratibu nitazoea EPL. Yeyote anayenifahamu, analifahamu ilo.
“Katika umri wa miaka 36, nimekuja kucheza kwenye ligi bora duniani. Kawaida hii ni ligi ya wachezaji vijana, lakini nimekuja kama mchezaji mzee. Ninaiona hivyo kwasababu Lampard na Chelsea wamehitaji uzoefu wangu.
“Kama mtu anapendelea mkimbiaji, basi ninaungana na alichosema Ancelloti kwa James ‘ kama unataka mtu mwenye mbio, wangemsajili Usain Bolt'” amesema Thiago Silva.
FURAHIA KASINO YA MTANDAONI
Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.


felister
kweli kabisa ngo’mbe hazeeki maini
Theckla
Umenena
Dorophina
Thiago yupo sahihi ingawa umri umeenda lakini bado miguu unafanya kazi ipasavyo
Mwanahamisi
Thiago yupo sahihi
Sauda
Maneno ameyatupa, tena yana ukweli ndani yake
Frank P
Namba za 365days ajidanganye hvy hvy epl ile
Latifa juma mohamed
Umenena hakika.
farida ahmadi
Kweli kabisah
Adelta
Yupo sahii
Nasra
Safii
Mwajumah
Safi
Fatuma kasomo
Gud news
Caroline
Pamoja na umri alionao lakini mbona ana kiwango kizuri
Angelina
Ni kweli
Fatina
Nice
Tahiya
Ama kwa hakika uko sahihi
Salma ngende
Kweli kabsaa
Rose kapinga
Thiago uko sahihi umri hausababishi kufanya vibaya iko kipaji umebarikiwa piga kazi tuu achana na namba ata kwenye viatu zipo!!!
Samiah
Kweli kabisa
magdalena
thiago analolisema lipo sahihi kabisa maana uwezo ndo kitu kikubwa sana katika soka
Hopemwaikuka
True say
Zeiyana
Thiago yupo sahihi japo kua mri hunaenda lakini hana mengi ya kufanya clabuni pale
Gabriel
Thiago yupo sahihi
Saupha mohamed
Ni kwelii
aisha
Thiago mtu mbaya
Khadija
Kweli umri ni namba hauzui kufanya mambo mengine
Amiri Kayera
Thiago ni beki mwenye uwezo
Issa
Kwa uwezo alionao ana uwezo wa kucheza miaka hata mi 5 zaid
Sabrina
Thiago silva yupo sahihi
Rehema
Safi
Ernest
Ngoja aonje joto ya jua ya Uingereza alafu tutamjaji vizuri sasa hivi hatuna cha kusema
Lydia Emmanuel Magoti
Ni kweli
Tatu
Umri si tatizo umri no
David Pere
Pamoja na umri alionao lakini mbona ana kiwango kizuri