Katika pita pita zangu mtandaoni nikakuta post yenye picha ya Clatous Chama iliyopostiwa na Deo mwanasoka ikigusia taarifa za wanasoka nguli duniani na ambavyo pesa imeweza kubadiri matakwa ya mioyo yao na kwenda pesa ilipo.

Kwenye post hiyo kunaonenasha dhahir kua lile linaoendelea mtandaoni kumuhusisha Clatous Chama kujiunga na Mahasimu wakubwa wa timu ya Simba Sports Club yenye makao yake makuu eneo la msimbazi jijini Dar es Salaam, ingawa taarifa hizo za Clatous Chama kujiunga na klabu ya Yanga Africa bado hazijarasimishwa,
Kwanini Tunafananisha Tukio la Chama na Yaliyopita
2013 Brazil wakiwa bize kuandaa kombe la dunia, kocha Luis Felipe Scholari aliulizwa anafikiria kumuita nani akaongoze safu yake ya ushambuliaji sambamba na Neymar Jr? Scholari alijibu kwa madaha na kebehi ‘The animal of Calderon-Diego Costa’.
Diego Costa alizaliwa na kukulia Brazil, aliondoka kwenda Ulaya akiwa na miaka 17. Hadi hayo maneno yakitoka katika kinywa cha Scholari, Costa alishaichezea Brazil mara mbili.

Wakati Brazil wanafikiria kuunda timu inayomzunguka Costa, Hispania walipita mlango wa uani na kumuwekea Diego ‘cheki’ juu ya meza yenye thamani ya kununua kisiwa chochote Hispania.
Costa alibadilisha mawazo ndani ya dakika mbili na kuamua kulikana taifa lake, akachagua kuitumikia Hispania. Mpaka leo wabrazil wanamuita ‘The Traitor’. Lakini Diego yeye hajali! Tayari pesa ilishasoma kwenye akaunti yake.
Baada ya Lorenzo Sanz kuiteka mioyo ya mashabiki wa Real Madrid, alikuwa na hakika kwamba anakwenda kushinda urais kwa mara nyingine. Ghafla alitokea Fiorentino Perez kusikojulikana kumpa changamoto.
Perez aliahidi kumshusha Luis Figo Real Madrid iwapo atashinda urais. Watu walimuona Perez kichaa asiye na jalala, Luis Figo aliyekuwa mchezaji bora wa dunia anayekipiga Barcelona anawezaje kusajiliwa na Real Madrid? Ila Perez alikuwa na mahesabu yake. Aliahidi kuwalipia viingilio vya msimu mzima mashabiki wa Real Madrid iwapo kama atakuwa rais na kushindwa kumsajili Figo.

Perez alikuwa na mahesabu yake, alishamuweka Figo kwenye mtego wa pesa kabla hajatoa ahadi yake. Na kweli mwaka 2000, Perez alimshusha Figo Real Madrid. Barcelona hawakuamini macho yao. Mpaka leo pale Barcelona wanamuita Figo, Yuda Iskariote. Hadi waliwahi kumlenga na kichwa cha nguruwe.
Labda hizi stori zinaweza zisihusiane na picha iliyopostiwa na mwanadishi Nguli wa Habari za michezo bwana Deo Mwanasoka, Lakini wahenga wanasema Lisemwalo Lipo na Kama Halipo basi Linjiani.
Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!



Mwajumah
Bora tu chama abaki simba maana uko anakotaka kwenda hakumfai wala sio level yake chama kwenda yanga
Carolyn
Ha ha ha tunasubiri muamuzi wa mwisho.yetu macho…Haji ataambia nini watu
Angelina
Nice update
Magdalena
Tunasubiri wakati ufike ndo tutaona Maamuzi yake Ni yapi kubaki au kusepa
Adelta
Maamuzi ni yake mwenyewe
Samira
Chama ni mali ya Simba hao utopolo watuache
Tatu
Yanga wanataka walipize ya morrison tatizo mkwanja wanao
Dorophina
Chama ndio mtu wa mwisho kutoa maamuzi wapi anahitaji kwenda hao wengine wanapiga upatu tu
Elika
Mchezaji kama mchezaji yeye ndo mwenye maamuzi yakufanya na kuamua aende wapi,sasa chama yeye ndo ataamua wapi pa kwenda
Fatina mfingi
Tatizo sio cham kwenda yanga ila pesa ya kutosha mnayo!
Fatuma kasomo
Uamuzi niwake
Khadija
Maamuzi anayo yeye asiumize watu vichwa
Saupha mohamed
Abaki tu simba
Sabrina
Abaki tu simba yanga hatuna shida nae
felister
uamuzi ni wake
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif meridianbet
Ester jackson
Uwamuzi ni wake kwenda yanga au kubaki mana yeye ndio anae yuwa wapi aende
Rahma
Nice
Shani
Chama ni mmoja tu
Zeiyana
Maneno hayo hayo yalisikika kwa Morrison kwenda simba kila mchezaji hana nafasi yake ya kuchagua sehemu sahihi hapa tunasubiri kuona mahamuzi yake chama
Povel
Hapo ni maamuzi yake kubaki kuendeleah Simba au kwenda utopolo fc
Issa
Chama asipokua makin na hiv vilabu vitamuulia soka lake mapema kama akina kichuya