Klabu ya Barcelona imeripotiwa iko mbioni kumshtaki nyota wake wa Zamani Neymar kwa kile wanachokiita ni kumzidishia malipo kwa zaidi ya Euro milioni 9 alipokuwa Barcelona.

Inakumbukwa nyota huyu wa PSG tayari alishalazimishwa kurejesha takribani Euro milioni 5.9 ambazo pia zilionekana kuwa ishu kwenye masuala ya bonasi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa The Sun, Barcelona walifanya hesabu vibaya za makadirio ya malipo ya Neymar na Kodi kwa miaka miwili ya awali na kujikuta wakilipa zaidi ya ilivyotakiwa.

Taarifa zaidi zinaripoti Wakala wa Kodi wa Barcelona tayari wametoa neno kwa Barcelona kuwa ikiwa watashindwa kufikia muafaka suala hilo, basi €9m itachukuliwa kama ni pesa ‘waliyojitolea kwa Neymar’ kama zawadi tu.

Huu ni muendelezo wa migogoro iliyoripotiwa kati ya pande hizi mbili. Mwezi Januari, Neymar aliripotiwa kuwa yeye ndiye anawashtaki Barcelona kwa takribani €3m – ambazo ni sehemu ya mshahara wake ambayo haijalipwa.

Baadala yake, taarifa mpya zinawataja Barcelona wakitaka kurejesha mara tatu ya pesa ambayo Staa huyu alitajwa kudai.

Sakata hili kwa upana wake linaihusisha na klabu ya Santos, ambayo Neymar aliondoka kuelekea Barcelona. Sekeseke hili pia halimuachi salama aliyekuwa raisi wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anayeshutumiwa kwa udanganyifu wa kodi na rushwa.

Suala hili linaibuka wakati Barcelona wakiwa wanajaribu kuweka sawa vitabu vyao vya fedha baada ya kupata changamoto kubwa ya kiuchumi kutokana na janga la Corona.


 

UMEJARIBU HII POKER YA VIDEO?

Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!

Meridianbet Casino

INGIA MCHEZONI!

21 MAONI

  1. Barcelona mmepotea sasa mnaaza sababu nyingine tu hizo zisizo na mashiko siku zote hizo mlikuwa wapi hasaivi ndio mnamuona yuko vizuri ndio mana mnaingiza maneno yenu muacheni nerymaa ale good time yake vema

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa