Miamba ya soka la Hispania – Barcelona bado hali ni tete kwenye suala la mishahara ya wachezaji. Waswahili wanasema “Hakatwi mtu hapa!!”, suluhisho ni nini?
Barcelona imeripoti hali mbaya ya kiuchumi inayoikumba timu hiyo kwa sasa kutokana na mlipuko wa COVID19. Kama sehemu ya kuendana na hali, uongozi wa timu hiyo ulilenga kupunguza mishahara ya wachezaji kwa takribani 30%.
Kama sehemu ya kutafuta suluhisho la hali hiyo, kulikuwa na vikao vingi kati ya uongozi wa Barcelona na wawakilishi wa wachezaji katika kujadili suala hili. Mpaka kufikia jana, Novemba 11, 2020. Hakuna maridhiano kuhusu kupunguza mishahara ya wachezaji.
Taarifa rasmi kutoka Barca inasema “Leo, Novemba 11 baada ya vikao vingi, na majadiliano yasiyo na kikomo, hakuna maridhiano yaliyofikiwa na pande zote. ”
Pande zote zinazohusika katika hili zimejiwekea ukomo wa mchakato huu kuwa ni Novemba 23. Lengo kubwa la Barca ni kupunguza mishahara ya wachezaji hasa wanaolipwa mkwanja mrefu kwenye kikosi hicho – Lionel Messi akiwa ni mmoja wapo.
Tayari baadhi ya wachezaji nyota kama Luis Suarez, Ivan Rakitic na Arturo Vidal wameshaondoka kwenye klabu hiyo ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa LaLiga.
Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!



Elika
Duh kwa upande wa wachezaji hali si ni mbaya sana..na hili janga la Corona na limemaliza kila kitu,Corona sio poa
Dorophina
Klabu nyingi zimeyumba kiuchumi mishahara ya wachezaji imekuwa gumzo kubwa corona imeharibu mambo mengi na uchumi
Magdalena
Kuyumba kwa uchumi si kilio cha Barcelona pekee Ni kilio cha club nyingi sababu ya gonjwa LA corona na swala LA usajili
Adelta
Uchumi umeyumba Corona sio pouwa
Fatuma kasomo
Duh sio Poa
Lydia Emmanuel Magoti
Duu mpaka kiereweke
Khadija
Mh!!!mbona makubwa
Tatu
Uchumi umeyumba dunia nzima kutokana na corona
Saupha mohamed
Uchumu umekua atali sana
Angelina
Corona imesababisha uchumi kushuka sana
Mwajumah
Duuh sio pow
Carolyn
Uchumi umeyumba kona zote
Sabrina
Hali ishakua tete uchumi umeyumbaa
felister
duh sio poa
Janeflora malisa
Kwa kwel hata uku hali ndio hiyo hiy
Ester jackson
Janga hili ni karibia timu zote kiuchumi wakovibaya zaidi nikuvumilia hali mpaka itakapo kuwa sawa
Rahma
Duhu sio poa
Shani
Barca imeyumba kiuchumi sabab haijauz wachezaj
Zeiyana
Kinachotakiwa wachezaji wakubaliane tu na ali hiliyokuwepo hakuna pa kukukimbilia kila clabu umekua na ali hiyo hiyo
Povel
Mlipuko wa corona umesababisha vilabu kuporomoka kwa uchumi dunian
Issa
Barecelona ni klabu ambayo imetetereka kimapato baada ya kukosa ligi na champion league