Tetesi zinasema Kiungo wa kati wa AC Milan Mturuki Hakan Calhanoglu, 26, huenda yuko njiani kuelekea Atletico Madrid baada ya mazungumzo ya mkataba na klabu hiyo ya Italia kukumbwana tatizo.
Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba anasema kwa sasa anapitia kipindi kigumu sana cha kazi yake ya soka kutokana na muda wake wa mchezo katika Old Trafford.
Tetesi zinasema Chelsea tayari wamekwisha kubali mkataba wa kumuuza midifilda wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 26, kwa Napoli wakati uhamisho wake wa mkopo utakapomalizika mwishoni mwa msimu.

Manchester City wanasaini mkataba na mshambuliaji ambaye ni kipaumbee chao cha mwaka 2021, nyota wa Borussia Dortmund Mnorway Erling Haaland, 20, na kiungo wa mbele wa Inter Milan Muargentina Lautaro Martinez, 23, ambao ndiye wachezaji wanaowalenga zaidi.
Mchezaji wa safu ya ulinzi ya Chelsea Mjerumani Antonio Rudiger, 27,yuko makini kuhusu kujiunga na klabu ya Barcelona wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari baada ya kupoteza nafasi Stamford Bridge.
Tetesi zinasema Mkurugenzi wa mchezo wa Liverpool Michael Edwards ameripotiwa kuamua dhidi ya kumuhamisha mlinzi wa Napoli Msenegal Kalidou Koulibaly, 29 msimu huu kwasababu ya pesa anazotaka alipwe.
Mkufunzi wa zamani wa RB Leipzig Ralf Rangnick anaamini kuwa kiungo wa safu ya kati-nyuma Dayot Upamecano, 22, ambaye Liverpool wanamlenga kumchukua, anaweza kuleta mafanikio Bayern Munich.

Juventus wako tayari kumnunua nyota mchanga anayechezea Ajax Ryan Gravenberch lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Barcelona katika kumsaini kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 18.
Mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa Kevin Phillips anaamini kuwa meneja Dean Smith anapaswa kumshawishi mchezaji wa safu ya kati anayeichezea Chelsea Muingereza Ross Barkley, 26 ,kwa mkataba wa mkopo kusaini mkataba wa kudumu na klabu hiyo.
Tetesi zinasema Vilabu vya Liverpool na Everton vinataka kumsajili mlinzi wa kati wa kibrazil anayechezea Torino, Gleison Bremer, 23.
Manchester United imeonywa na wakala wa Eric Bailly kwamba mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Ivory Coast huenda akafikiria upya mustakabali wake kama hali ya sasa ya kucheza muda mchache haitabadilika.
Mmeneja wa Tottenham Jose Mourinho amesema mkataba wa mkopo wa kiungo Gedson Fernandes, 21 kutoka Benfica unaweza kufikia kikomo January.
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.



Elika
Bakayoko kama ataelekea napol itakuwa vizuri sana
magdalena
mpaka pogba kaamua kusema mara nyingi kweli anapitia kipindi kigumu pale united sababu ya kukalishwa benchi kwa muda mrefu na kuoewa muda mchache wa kucheza
Lydia Emmanuel Magoti
Itakuwa poa kiungo huyo akielekea kwenye timu hiyo hatakuwa amelamba dume Anajua
zeiyana
man u waliangalie ilo pogba amepoteza ule mvuto wa zamani ukiangalia pogba amekua kama mchezaji tegemezi clabuni hapo pasipo hata na msaada wa mchezaji kazi nyingi hanazo zimefanya zimemfanya hapungue kiwango chake
Carolyn
Pogba ana wakati mgumu sana.pole sana
ester jackson
Bakayoko kwa kipindi hichi ameonekana kiwango chake kimeshuka ndio mana Chelsea wanataka kumuuza ili wasajili wachezaji nguli wenye matamanio zaidi ya mafanikio
Fatina mfigi
Asanteh kwa makala!!
Adelta
Bakayoko anatakiwa kuongea juhudi ili awe kwenye kiwango Bora
Rahma
Shukrani kwa makala
Hopemwaikuka
Pole Paul Pogba ni mapito tu
Angelina
Nice update
Mwajumah
Pogba anawakati mgumu sana
Povel
Nice update
Sadick
Ni wakati wa Pogba kuondoka Man U na kujaribu maisha mahali pengine
Issa
Pogba mawazo na akili yake vipo madrid hiyo inachangia kushuka kwa soka lake
aisha
Akaze buti la sivyo mpira unamuacha maana mpira ni akili na kutulia kwenye game
Sabrina
Itapendeza sana Antonio akitua Barcelona
Sauda
Pogba kazi anayo
Saupha mohamed
Pogba kazi anayo