Erasto Nyoni, Beki wa Kiwango cha Lami Tanzania

Kuna kipindi nilitumia muda mwingi sana kujifunza kuhusu wachezaji bora waliowahi kutokea duniani, kuna wakati nilikesha usiku nikitafiti juu ya mabeki waliopita katika soka. Nilisoma vitabu, nikatazama video na kuuliza. Niamini mimi kuhusu mabeki, wanasifiwa kuwa bora kwasababu ya ukatili, ugumu na ukorofi.

Katikati ya maandishi nilikutana na jina la Nemanja Vidic wa Yugoslavia, huyu alikulia katikati ya vita, milio ya risasi na magari ya vita yalikuwa mziki wake, moshi wa mabomu ulikuwa chakula chake. Alistahili kuwa mkatili.

Nilikutana na jina la Jaap Stam. Huyu ni muholanzi mwenye damu ya Italy, nchi mbili zinazosifika kwa kuzalisha mabeki wagumu na korofi. Ukabaji wa giza ulizunguka ndani ya mwili wa ‘BIG JAP’.

Mara lilitokea jina la Fernando Couto, serikali ya Ureno iliwahi kumshitaki kwa matumizi ya madawa ya kulevya kisha wakampa dhamana ili akaitumikie timu ya taifa. Hakuigiza ukabaji wa kikatili, maisha yake yalisadifu ukatili.

Imeandikwa mabeki wagumu wanatoka katikati ya historia ngumu. Sikushangaa kusikia Mathias Sammer aliwahi kuwa kibaka.

Kama mvua katikati ya kiangazi lilitokea jina la Fabio Cannavaro. Katikati ya Waitaliano walioamini mpira ni vita yeye alikuja kuwaaminisha akili inaweza kucheza mpira kuliko nguvu. Licha ya umbo lake dogo aliwadhibiti washambuliaji nyumba, aliokoa mipira ya hewani na kushinda mabao ya vichwa. Mpaka leo waitaliano wanakiri hawajawahi kumuona kitasa kama yeye.

Jioni moja pembeni ya mzee Mfinga tukipiga stori aliniambia juu ya mtu mmoja Salum Kabunda. Mnara wa babeli uliosimama kwenye ukuta wa Yanga Afrika 1988, kutokana na sanaa nyeusi ya ukabaji aliyoitumia, Yanga Afrika waliamua kumuita Ninja.

Kisha akanieleza juu ya George Magere Masatu, mnyonyoro uliofunga geti la Simba miaka ya 90. Majina ya vitasa yalienda kumiminika, Ahmed Amasha, Athuman Juma Jogoo, Rashid Idd Chama, Rueben Mgaza na wengineo.

Mara akatajwa Nadir Haroub Cannavaro. Wazanzibar nao wanayo beki anayeiamini akili kuliko nguvu. Katikati ya Victor Costa na Salum Swedi alichomoza kama uyoga. Erasto Nyoni naye alikuja hivi…

Itaendelea..


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

18 Komentara

    nyoni ni beki mzuri sana ata timu anayoichezea inajivunia kuwa na yeye

    Jibu

    Nikweli kabisa elasto nyoni nikiungo mkabaji Mwenye maguvu yake akikaa kwenye sekta yake apatoshi namkubali kiungo mshambuliaji huyo

    Jibu

    Mda wake huu nyoni wa kuonesha uwezo wake

    Jibu

    Erasto nyoni hongera kwa kufanya investigation.ila upo vizuri

    Jibu

    Beki makini ni muda wake kutupa unafuu Wa maumivu ya kufungwa tunataka juhudi zake zaidi siku ya kesho ili ituwekee njia ya kupita watanzania kila LA heri kwenye mchezo Wa kesho

    Jibu

    Beki wa kutumainiwa kbc

    Jibu

    Nyoni ni beki mzuri na anajuwa majukum
    Yake

    Jibu

    Nyoni ni beki mzuli mno mda wake wa kuonyesha ujuzi wake

    Jibu

    Dah! nasubir muendelezo

    Jibu

    Yuko vizur

    Jibu

    Namkubali sana yupo vizuri

    Jibu

    Erasto nyoni ni mmoja ya vizazi bora vya soka nchini tanzania ni muhimili mkubwa Sana katika soka la tanzania

    Jibu

    Erasto Nyoni ni bonge la beki wa kulia. Nashangaa Kocha wa Simba hamuchezeshi mara kwa mara

    Jibu

    Nyoni amekua bora sana sema kocha wa simba hana mpango nae

    Jibu

    Nyoni yuko vizuri sana

    Jibu

    Erasto Nyoni anajituma sana uwanjani

    Jibu

    Nyoni anajituma sana

    Jibu

    Nyoni yupo vizuri

    Jibu

Acha ujumbe