Kiungo wa Ferencvaros, Marcel Heister amedai kuwa aliomba kubadilishana jezi na Cristiano Ronaldo lakini nyota huyo wa Juventus alitupilia mbali jambo hilo mara baada ya mchezo wao wa Ligi ya mabingwa ulaya.
Ronaldo alicheza dakika zote 90 katika kikosi cha Andrea Pirlo kilichoibuka na ushindi wa bao 4-1 huko Hungary mno Novemba 4.

Lakini Ronaldo hakufanikiwa kupata bao kitu ambacho kinamfanya Heister aamini kuwa ndiyo sababu ya Ronaldo kukasirika na kumnyima jezi.
Akiongea na SPOX Alidai kuwa “Alionekana(Ronaldo) mwenye gadhabu na hasira kiasi, labda kwa sababu hakutufunga goli, ama kwa sababu nilimkaba na kumpokonya mpira alipotaka kunipiga chenga.”
Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.



magdalena
ronaldo ajaonesha uungwana
Rahma
Nice
Ester jackson
Nafikiri amefanya jambo Jena kwake mana kama angempa ingemlazima kufukiwa timu kucheza au adhabu kutokana na sheria zilizowekwa na uongezi kwa kipindi hiki cha corona ina walazima wachezaji kutobadilishana jezi
Sauda
Siyo poa Ronaldo.
Shakila mrope
Ronaldo ni mbinafsi
Dorophina
Hayo yalikuwa ni maamuzi yake ronaldo kumpa au la kutofunga sio sababu
Mwajumah
Apo cr7 amezingua hajafanya uungwana kabisa
Adelta
Ronald Yuko vizuri
Angelina
Ni uamuzi wake kutoa au kutokutoa ajikaze tu
Caroline
Ronaldo pengine hataki kushare.corona hii wasije kuambukizana
Sania
Ronaldo apunguze ubinafsi
Nasra
Kazingua sana katika hili
Khadija
duuh jamaa anaimani mbaya sana yani kukataliwa kubadilishana jezi kashafikilia vibaya
Fatina mfingi
Mmmh. Imezingua broo
Hopemwaikuka
Anajikuta nan sasa
aisha
Duuuh ebwanaeee huyu ronaldo sijui anajikuta nani aisee
Povel
Cr7 ni mwamba asiye kuwana na majivuno katika kulisaka kabumbu
Saupha mohamed
Ronaldo MTU mbayaaa
Issa
Ronaldo alifanya ili kuepuka maambukizi ya corona
Sadick
Ni heshima kuwa na Jezi ya Ronaldo au Messi kabati kwako. Amekuwa akitoa Jezi kwa wengi nadhani Heister hakuwa na bahati siku hiyo
Gabriel
Nice upadate 👍
samiah
Nice
Tatu
Ronaldo ajafanya poa
Lydia Emmanuel Magoti
Ronaldo alivyo fanya sio fea
Sarah
Sio vzr ronaldo
warda
Hata mie nisingebadilishana nae kwa kweli
Chiku
Hicho nacho kipengele