Anthony Joshua anajiandaa kuingia ulingoni dhidhi ya Kubrat Pulev Disemba 2, 2020. Hili linakuwa ni pambano lake la kwanza tangia alipopambana Andy Ruiz mwaka uliopita.

Bondia huyu wa miaka 31 ana historia nzuri ya kushinda mapambano akiwa na rekodi ya 23-1 katika mapambano yake ya ndondi za kulipwa.

Anthony Joshua anamiliki mataji ya ubingwa wa dunia IBF, WBO na WBA, huku akiendelea kuiwinda ubingwa wa WBC unaomilikiwa na Tyson Furry.

Kwenye rekodi yake ya mapambano, pambano dhidi ya Ruiz ndiyo pambano pekee alilopoteza. Ni bondia amayefahamika kwa umakini mkubwa katika mapambano yake 24, mapambano 21 ameshinda kwa KO, mawili kawaida huku akipoteza hilo moja tu.

Anthony Joshua

Aliyekuwa mkufunzi wa Andy Ruiz, Manny Robles ameweka wazi mbinu za Kumtandika Anthony Joshua.

“Mkono wa kulia. Ikiwa utatumia mkono wa kulia vizuri na kumtupia ngumi kifuani, Ngumi mwilini na kurejea kwa mkono wa kulia, hapo ndipo ninahisi Joshua anakuwa kwenye mazingira magumu.

“Umeona katika pambano la Povetkin, ni nani alieyetandika kwa mkono wa kulia. Wapiganaji wengi ambao wameweza kumuumiza Joshua – umekuwa mkono wa kulia.”

Unafikiri mbinu hii inaweza kunufaisha Pulev katika maandalizi ya pambano lake na AJ? Achia maoni yako hapo chini.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

8 MAONI

  1. Antony joshua hawez kupgika Kama wengi wanavyotegemeak kirahis hvy kwa kuwek mbinu hadharani ila ngoja tuone mchezo wa masubwi hau tabilik yoyote alijiandah vzr hanaweZ kuwa mbabe katika pambano hilo kila la kheri

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa