Waswahili husema ‘nabii hakubaliki nyumbani’. Ukitaja Bruno Fernandes ukiwa Ureno, sio wengi watakaoshtuka kama utakavyosema Cristiano Ronaldo. Ila mtaje Fernandes ukiwa Manchester na utapigiwa makofi kwa shangwe kubwa kutokana na uwezo wa kiungo huyo.

Bruno Fernandes afunguka kuhusu kumpatia Marcus Rashford penati licha ya kwamba ilikuwa ni nafasi yake kupachika ‘Hat-trick’ kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa na Man United.

Mchezo wa 4 kwenye hatua ya makundi kunako Ligi ya Mabingwa, Man United walikutana na Istanbul Basaksehir katika mchezo wa marudiano baada ya kupoteza mchezo wa kwanza.

Alikuwa ni Bruno Fernandes aliyepeleka shangwe kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kupachika magoli 2 ndani ya dakika 20 na mchezo ulimalizika kwa ushindi wa 4-1.

Bruno Fernandes, Bruno Fernandes Atoaneno Kuhusu Penati, Meridianbet
Fernandes amehusika kwenye magoli 34 (magoli 21 na pasi 13 za magoli) kati ya mechi 35 alizoitumikia Man United.

Bruno Fernandes alikuwa na nafasi ya kupachika goli la tatu lakini aliamua kumuachia Rashford jukumu la kupiga penati kunako dakika ya 35 na muingereza huyo hakufanya makosa, alipachika goli la 3.

Akizungumzia uamuzi huo, Fernandes amesema “ni kweli kila mchezaji anataka ‘hat-trick’ lakini baada ya mchezo wa EPL (dhidi ya West Brom) nilimwambia Rashford atapiga yeyote itakayofuata.

“Lakini pia ni miongoni mwa wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa kwa hiyo ni muhimu kwake kuendelea kujiamini zaidi.

“Haijalishi ni nani anapiga penati, kitu cha muhimu ni ushindi”

Kocha Ole Gunnar Solskjaer naye alikuwa na chakusema kuhusu uamuzi wa Fernandes. Ole amenukuliwa akisema “Marcus ni mpigaji mzuri wa penati na Bruno anajiamini sana, kama Bruno alitaka kumpatia Marcus sasa kwanini asifanye hivyo? Anthony Martial alipiga kwenye mechi dhidi ya Leipzig – sasa kwanini wasishirikiane?

Huu ni mchezo wa kwanza kwa United kuongoza kwa magoli 3 kabla ya mapumziko kwenye Ligi ya Mabingwa. Mara ya mwisho walifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Roma (7-1) mwezi Aprili, 2007.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

26 MAONI

  1. Man U imekuwa ikipata penati karibia kila mchezo jambo ambalo linashangaza wengi. Bruno ni mpigaji mzuri wa Penati na alikuwa muungwana kumwachia mwenzie

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa