Baada ya kuweka rekodi sawa na bingwa mara 7 wa mbio za langalanga – F1 (Michael Schumacher), Andy Murray anasema Lewis Hamilton anastahili kuungana naye kama wanamichezo wenye heshima kubwa Uingereza.

Kunataarifa kuwa Lewis Hamilton atatunukiwa cheo cha ‘knighthood’ kwenye New Year Honors. Hizi ni tuzo ambazo zinatolewa na Malkia wa Uingereza – Queen Elizabeth II.

“Kwa mafanikio aliyoyapata kama mwanamichezo, anastahili. Ni kati ya wanamichezo waliofanikiwa zaidi kwenye historia ya nchi hii.” Murray ameiambia Good Morning Britain 

Andy Murray Alipotunukiwa Cheo cha Knighthood mwaka 2017.

Andy Murray ambaye alitunukiwa cheo hicho 2017, aliongeza kuwa “anasaidia mambo mengi nje ya uwanja, kwahiyo ninaweza kusema anastahili tuzo hiyo kulingana na mafanikio yake.”


Lewis Hamilton alitunukiwa tuzo ya MBE mwaka 2009, siku za karibuni alimwambia Sally Nugent wa BBC kuwa “itakuwa ni siku yake ya furaha sana kama atapata nafasi ya kutunukiwa tuzo na Queen Elizabeth II kwa mara nyingine”.

Hamilton Alipotunukiwa tuzo ya MBE na Queen Elizabeth II mwaka 2009.

Wiki iliyopita, Bingwa wa F1 mwaka 1996 – Damon Hill alisema Lewis Hamilton amevunja vizuizi vingi kupitia mafanikio yake.

“Cheo cha knighthood haitokuwa ni utambuzi wa udereva wake tu, lakini pia ni kama dereva mwenye rangi nyeusi ambaye amefungua milango kwa watu wengine ambao sio weupe.

“Ameondoa utamaduni wa kuwa hiki hakiwezekani, kwamba kunamaeneo huwezi kufanikiwa kutokana na rangi ya ngozi yako. Ameondoa kabisa huo mtazamo.”


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI


28 MAONI

  1. Lewis Hamilton anasitahili pongezi nyingi kwa dhamira yake isiyoyumba kutafuta mafanikio na akayapata. Vikwazo vilichochea nia yake ya kusonga mbele kwa kasi zaidi. Ni moja ya mashindano magumu zaidi na ya kuvutia

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa