Ulimwengu wa soka na mashabiki wa Real Madrid kwa upekee wao, wanautambua uwezo wa Luka Modric katika safu ya kiungo.

Mkataba wa Luka Modric unamalizika mwishoni mwa msimu huu na hakuna dalili kama anaweza kuongezewa mkataba mpya mpaka sasa.

Licha ya kutokuwa na dalili za mkataba mpya, Modric amefunguka kuwa anataka kuendelea kuwepo Madrid na ameenda mbali zaidi kwa kuongeza kuwa atakuwa mwenye furaha zaidi kama atapata nafasi ya kustaafu maisha ya soka akiwa Santiago Bernabeu.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter Milan leo usiku, Luka Modric amesema ” Nimesema hili (kwamba ninataka kubaki Real Madrid) mara nyingi lakini tusubiri tuone nini kitakachotokea. Kila mara ninatoa jibu lilelile, ninajisikia vizuri na ninataka kuendelea kuwepo Madrid.

Luka Modric, Luka Modric Kustaafia Madrid, Itawezekana?, Meridianbet
Luka Modric

“Ninahisi ninaweza kuisaidia timu, kama utaniuliza ni nini ninahitaji, ninahitaji kubaki. Ninataka kumaliza maisha ya soka nikiwa hapa lakini hilo litategemea mambo mengi. Hakuna mtu atakuwa mwenye furaha kunizidi mimi kama nitastaafia hapa.

“Ninajisikia vizuri. Michezo ambayo sikucheza ni kutokana na maamuzi ya kocha na ninapocheza, ninajaribu kufanya vizuri.

“Wanaongelea sana hali yangu lakini tusubiri tuone ni nini kitatokea mbeleni.”

Je, Real Madrid watachukua uamuzi wa kumbakiza Luka Modric klabuni hapo au wataamua kuachana naye mkataba wake utakapo malizika? Madrid wameanza vibaya Ligi ya Mabingwa msimu huu wakiwa wameshinda mchezo 1 kati ya 3. Ushindi dhidi ya Inter leo usiku utawapa matumaini ya kuendelea kusalia kwenye Mashindano ya msimu huu.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

27 MAONI

  1. Kiwango Modric kimeshuka na Madrid inatakiwa kusajiri wachezaji wenye viwango kuendelea kubaki ktk ubora na Kocha anamuona hana msaada tena ndio maana anamuweka bench

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa