Usajili wa Donny Van De Beek haukutarajiwa miongoni mwa mashabiki wengi wa Man United. Licha ya kucheza mechi chache, Donny ni kama anaendelea kuonesha ubora wake ndani ya United.

Kwenye Ligi ya Mabingwa, Van De Beek amecheza mechi zote za Man United (4 mpaka sasa) katika nafasi mbalimbali. Mchezo dhidi ya Istanbul Basaksehir Donny alicheza kama namba 8 akisaidiana na Fred aliyecheza kama kiungo mkabaji.

Ni kati ya michezo ambayo kiungo huyo raia wa Uholanzi ameendelea kuonesha uwezo wake mkubwa wa kutawala mchezo na kuongoza mashambulizi. Anazitumia vizuri nafasi anazozipata na pia anatengeneza nafasi kwa wachezaji wengine awapo uwanjani.

Van De Beek, Van De Beek Anaendelea Alipoishia., Meridianbet
Donny Van De Beek akipambana na mchezaji wa Istanbul Basaksehir kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa.
Je, kuonesha kiwango safi kwenye michezo ya Ligi ya Mabingwa kutampatia Van De Beek namba ya kudumu kwenye kikosi cha Man United?.

Kocha – Ole Gunnar Solskjaer alizungumzia maendeleo ya Donny na Edinson Cavani ndani ya kikosi chake.

Akizungumza na BT Sports, Solskjaer alisema “wote wameanza kuzoea maelekezo ya namna tunavyowataka wacheze – Donny anaweza kucheza kwenye nafasi mbalimbali na Edinson ni namba 9 mwenye staili ya zamani, kitu ambacho hatukuwa nacho kwa muda na nilifurahishwa na namna Martial alivyocheza upande wa kushoto.”

Donny alipata nafasi ya kuzungumza na MUTV ambapo alisema “Ulikuwa ni mchezo mzuri. Kwenye baadhi ya michezo ninacheza namba 10, muda mwingine kocha ananihitaji nicheze katika nafasi za kuutawala mchezo, hiyo ni sawa kwangu, muda mwingine nilipokuwa Ajax nilikuwa ninacheza kwenye nafasi hiyo hivyo hakuna tatizo katika hilo.”

Donny anapambia namba katika kikosi cha Man United akichuana na wachezaji kama Paul Pogba, Bruno Fernandes, Juan Mata, Fred, Scot McTominay na Nemanja Matic katika orodha ya viungo wa timu hiyo.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

29 MAONI

  1. Van de beek ni mmoja ya viungo bora waliotokeah ndani ya united mashabik na wapenzi wa united wanategemeah makubwa kutokA kwa van de beek msimu huu

  2. Uzuri wa Ole kila mchezaji anayemnunua anamchezesha ingawa anakuwa hana uhakika wa namba. Man ilitakiwa kusajiri beki sio nafasi ya kiungo

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa