Bingwa mara saba wa WWE, The Undertaker, ameaga rasmi kuwepo katika mchezo huu maarufu wa mieleka baada ya kuwepo kwa miaka takribani 30.

Tumfahamu kidogo The Undertaker

Jina lake halisi anaitwa Mark William Calaway, na jina lake maarufu zaidi ni “The Dead Man” -kwa lugha za kule Buza ni mtu aliyekufa, au inakaa poa zaidi tukisema “Mzimu Fulani”. Alizaliwa mnamo Machi 24, 1965 kule Houston, Texas, U.S.

Amekuwa na uhusiano wa ndoa na wanawake watatu kwa nyakati tofauti Jodi Lynn ( Alimuoa 1989; Talaka 1999)​ Sara Frank ​ ​ (Alimuoa 2000; Talaka. 2007)​, Michelle McCool (alimuoa 2010 na yupo naye mpaka sasa)​. Utajiri wake unakadiriwa kuwa $22m.

Maisha yake na Mieleka!

The Undertaker amekuwepo kwenye mchezo wa mieleka kwa miongo kadhaa. Aliingia rasmi kwenye mieleka mwaka 1990 baada ya kusaini dili na kampuni maarufu ya World Wrestling Federation (WWF). Mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Kane Novemba 19, 1990.

Novemba 22, alicheza mechi yake ya kwanza kwenye WWE ya Survivor Series. Aliendelea kuwa bora na mshindani mkubwa siku hadi siku. Ni akribani miaka 30 sasa, tangia aingie kwenye mieleka mpaka kustaafu kwake

“Ni Muda wa Kupumzika”

Mastaa wengi sana waliowahi kuwepo WWE, akiwemo The Rock, Triple H na Vince McMahon walijumuika naye wakati akitoa neno juu ya hatma yake katika mashindano hayo makubwa ya mieleka duniani.

The Undertaker

Orodha ya waliokuwepo ulingoni kutoa sapoti katika salamu zake za mwisho ni ndefu, miongoni mwao ni Kevin Nash, Mick Foley Jeff Hardy, Shawn Michaels, Booker T, Triple H, The Godwins, Savio Vega, Rikishi, JBL, Shane McMahon, Big Show, Ric Flair, The Godfather na Kane.

The Undertaker anaamini WWE umempa nafasi kubwa ya kujijengea heshima. Anafahamika vyema kwa kuendelea kuwapa radha ya tofauti mashabiki wake na kujibu kujiweka katika namna tofauti kama watu wa anga ya mbali wenye nguvu ya tofauti na binadamu wa kawaida. Ni picha alivyopenda kuwajengea mashabiki wake.

The Undertaker
The Undertaker akichuana dhidi ya Goldberg (WWE), January 7, 2019. (Photo credit; AMER HILABI/AFP/Getty Images)
Akizungumzia safari yake na WWE, The Undertaker ambaye anaamini mda wake umefika amesema “Sasa ni muda wangu wa kupumzika”.

Hata hivyo, kutokana na ubora wake aliokuwa nao na mchango wake mkubwa kwenye WWE, ilikuwa inatarajiwa kuwa angepewa shughuli ya heshima kwa ajili yake tu na WWE. Lakini bado waandaaji hawajaweza sawa mpango huu katika kipindi hiki ambacho hali bado haijakaa sawa.


 

Usichelewe Kukamata Mkwanja Huu!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

 

26 MAONI

  1. Daaah Naukubali sana Undertaker kwenye action yake ya kuingia ulingoni katika kuangali upiganaji wake akiwa amempika mpezi wa victory basi mwanamama huyo aliamua kumlipa mtu wa kumpiga Undertaker alijaribu sana lakini wote alio wapa pesa walipigwa mwishoe akampata Jeff Hardy ambaye alifanikiwa kumpiga sana mpaka kumuweka ndani ya jeneza Jeff Hardy hapo ndipo nikajua kuwa a undertaker anambabe wake #meridianbettz

  2. undertaker ni ahaki yake kutaka kuuaga huu mchezo sababu umri wake umeshakuwa mkubwa sana ingawa mashabiki wake tulikuwa bado tuna uhitaji naye

  3. Vizuri Sana kwa uwamuzi alio uchukua pia umri umeenda ndomana kaongea kustaafu anataka kupumzika angalie yalio mbele yake ila undertaker alikuwa tishio Sana kwenye WWE alikuwa mtu atariii Sana namkubali akishuka pale namkoti wake duuu tishio sana

  4. Kuna watu huwezi kuwabandua kwenye TV wanapotaza mchezo huu, inasemekana Donald Trump ni moja ya mashabiki wa mchezo huu hatari.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa