Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah amerejea mazoezini kwaajili ya mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) utakaowakutanisha na Atalanta ya Italia uwanjani Anfield leo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alikosa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) iliyoshuhudia Liverpool wakiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Leicester City uwanjani Anfield Jumapili iliyopita.

 

Salah Fiti Kuwavaa Atalanta.

Salah alikosekana katika mchezo huo kutokana na ugonjwa wa Covid-19 alioupata wakati akiwa katika kambi ya timu ya taifa ya Misri iliyokuwa ikicheza na Togo kwenye mechi mbili za kufuzu kwa fainali za Kombe la Afrika (AFCON) mnamo 2022.

Katika mechi iliyopita ya UEFA, Liverpool waliwafunga Atalanta kwa magoli 5-0 jijini Bergamo, Italia na mechi ya leo itakuwa marudiano katika uwanja wao wa nyumbani Anfield, Uingereza.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

22 MAONI

  1. Jambo la kuvutia ni kwamba tunaanza kuishi na corona kama kawaida tofauti na awali tulivyokuwa tunaogopa mno. Karibu Dimbani Mo Salah

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa