Tetesi za Soka Barani Ulaya.


Tetesi zinasema mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc anatazamia kumuona mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland katika klabu hiyo kwa muda mrefu.

Nyota huyo aliye na miaka 20- ana mkataba na klabu hiyo ya Bundesliga hadi mwaka 2024, lakini anaweza kuondoka kwa euro milioni 75 (£67m) mwaka 2022 kwasababu ana kifungu kinachomruhusu kufanya hivyo katika mkataba wake wa sasa.

Klabu za Ligi ya Primia zimeombwa kupunguza idadi ya mashabiki wanaoruhusiwa uwanjani hadi 1,000. Mamlaka ya usalama wa viwanja vya michezo imesema agizo hilo linastahili kuzingatiwa kwa muda hadi pale mashabiki 2000 wataruhusiwa uwanjani.

Tetesi zinasema winga Muingereza Angel Gomes, 20, anasema aliondoka Manchester United kutafuta mwanzo mpya baada ya kukataa ofa yao na kujiunga na Lille.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Anderlecht Mbelgiji Marco Kana, 18, Liverpool ndio klabu anayotamani kujiunga nayo atakapoamua kuhama.

Kipa wa Fulham Marcus Bettinelli, 28, ananyatiwa na klabu kadhaa za Ligi ya Primia. Kipa huyo ambaye kwa sasa yuko Middlesbrough kwa mkopo, alijumuishwa katika kikosi cha kitaifa cha England na Gareth Southgate mwaka 2018.

Tetesi zinasema mshambuliaji wa Burnley na Jamhuri ya Czech Matej Vydra, 28, anataka kuondoka Turf Moor ili kupata nafasi ya kucheza soka ya kikosi cha kwanza.

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson, ameahidi kuongeza msaada wake wa chakula kwa shirikala la watoto na kutoa wito kwa wachezaji zaidi wa soka kumsaidia mshambuliaji wa England na United Marcus Rashford, 23, katika kampeni yake ya kuwakinga watoto dhidi ya njaa.

 

Nicolas Tagliafico

Beki wa kushoto na nyuma wa Argentina Nicolas Tagliafico, ambaye amehusishwa na Chelsea na Manchester City, amekubali kurefusha mkataba wake na Ajax ambayo inatarajiwa kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28- kusalia katika klabu hiyo hadi angalau mwisho wa msimu .

Tetesi zinasema mkurugenzi wa kiufundi wa AC Milan Paolo Maldini amekiri kuwa anamtaka winga wa Ufaransa Florian Thauvin, 27, ambaye mkataba wake Marseille unakamilika mwaka 2021.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 Komentara

    Tetesi zinasomeka kwa sababu beki amekubali kuongeza mkataba

    Jibu

    Alex Ferguson amefunguka kutoa msaada kituo cha watoto

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Iko poa

    Jibu

    Vizuri San

    Jibu

    Mpo vizuri kwa taarifa

    Jibu

    Haaland angetua EPL ingekua poa Sana

    Jibu

    Epl ingenoga angepatikana haaland

    Jibu

    Wakimpata haalad watakua wamepata dodo

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Ferguson safi

    Jibu

    Haaland yupo vizuri akikipiga Dortmund itakuwa poa sana

    Jibu

    Kana akienda Liverpool atakuwa ameenda katika kikosi bora kwake

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Nic

    Jibu

    Mkataba Mrefu balaa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.